May 11 2015 Kajala akionekana na jeraha lake juu ya jicho la kushoto kwenye meza ya Majaji wa shindano la vipaji Kinondoni Dar es salaam. |
May 10 2015 mwigizaji wa bongomovie Kajala
amekwenda kumsupport msanii Mabeste ambaye alifanya show New Maisha Club
kwa ajili ya kuchangisha pesa za kumsaidia mke wake kwenye matibabu.
Kajala anasema''Mpaka
tumemaliza show, sasa kwenye muda wa kuondoka nikamwambia Meneja wangu
amuite msanii wetu mmoja anaitwa Tausi ili tuondoke, sasa wakati nataka
kushuka kwenye gani natembea tu sijui chochote nikashangaa chupa
imenipiga usoni, nikadondoka na kubiringika kwenye zile ngazi, kuna
mkaka na mdada wakaniona wakanisaidia"
‘Aliyenipiga
na hiyo chupa ni Mwanaume, simjui na wala sijawahi kumuona hata mara
moja…. amekamatwa yuko Osterbay Polisi, nilivyotoka Maisha Club
nilipelekwa Hospitali Mwananyamala nimeshonwa usoni aliponiumiza,
tukarudi Polisi nikaandika maelezo‘ Kajala
Kwenye sentensi nyingine Kajala amesema ‘Huyu
Mwanaume aliulizwa pale Polisi anasema eti ni Pombe, lakini mtu eti
Pombe umeingizwa ndani saa moja tu unakumbuka kwamba ni pombe ndio
imekufanya hivyo? sio kweli….. itakua tu alidhamiria yeye mwenyewe’
Unaweza kumsikiliza Kajala akiongea yote mengine kuhusu hili tukio kwa kubonyeza play hapa chini….