Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo NEWS. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo NEWS. Onyesha machapisho yote

MAWAZIRI WAWILI WANUSULIKA KUTUMBULIWA NA RAIS MAGUFURI



 Operesheni ya kutumbua majipu ya Rais John Magufuli nusura iwaangukie Mawaziri wawili ambao  pia walikuwa  manaibu  mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Taarifa kutoka katika chanzo cha kuaminiwa zimeeleza kuwa Rais Magufuli alionesha kutoridhishwa na utendaji wa Mawaziri hao na kuwafokea mbele ya mawaziri wenzao  kwa kuwataja majina katika kikao maalum cha mawaziri kilichofanyika hivi karibuni.
"Ni mazingira ambayo mawaziri hawakuyazoea kwamba Rais anawaambia moja kwa moja kwa majina, anafoka akisema anaweza kuwafukuza wakati wowote.....
"Mawaziri wamezoea mara kwa mara wanapofanya kosa au uzembe wanaonywa kwa staili tofauti, ni kama ya kistaarabu hivi. Sasa huyu bwana mkubwa hana mchezo, aliwataja kabisa, tena mbele ya wenzao ambao walibaki vinywa wazi.

“Wewe (anataja jina la Waziri) na mwenzako (anamtaja jina pia) nitawatumbua,” Chanzo cha gazeti la Rais Mwema kinamkariri Rais Magufuli.
Mawaziri hao ambao ni wabunge wa kuchaguliwa majimboni kwa upande wa Tanzania Bara, wanaongoza wizara nyeti ambazo zinasimamia sekta mtambuka, wizara ambazo zinagusa sehemu ya ahadi za mabadiliko alizonadi Magufuli wakati akigombea urais katika kampeni za mwaka jana.

Chanzo hicho kilieleza kuwa Rais Magufuli aliwaonya pia mawaziri wengine ambao alionesha kutoridhishwa na utendaji wao kwakuwa hawaendani na kasi yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

“Magufuli alitaka atoe mfano kwa mawaziri wengine kwamba wao si watu maalum sana. Kama wanavyotumbuliwa watu wengine na wao pia wanaweza kutumbuliwa,” kiliongeza chanzo hicho

Rais Magufuli aliunda Baraza lake la Mawaziri mwishoni mwa mwaka jana na kuwashauri wasifanye sherehe ya kuteuliwa kwakuwa wakifanya vibaya hatawaonea haya atawaondoa mara moja bila kujali majina yao.

Utendaji wa Rais Magufuli umeendelea kusifiwa kila kona hususan katika kuwawajibisha viongozi wa ngazi zote na kuonesha nia ya dhati ya kuwahudumia watanzania huku akipambana na uzembe na ufisad
WATU 430 NCHINI INDIA WAAGA DUNIA KWA KUKUMBWA NA WIMBI LA JOTO KUBWA

WATU 430 NCHINI INDIA WAAGA DUNIA KWA KUKUMBWA NA WIMBI LA JOTO KUBWA

.
Takriban watu 430 wamekufa kutokana na wimbi la joto linalovuma nchini India.
Watafiti wamesajili kiwango cha juu mno cha nyuzijoto 48'C katika maeneo mengi nchini humo.
Vifo vingi zaidi vimeripotiwa katika majimbo ya kusini ya Telangana na Andhra Pradesh, ambapo watu 140 wamepoteza maisha yao kuanzia jumamosi wimbi hilo la joto lilipotokea.
Mji wa Allahabad ulioko Uttar Pradesh ulisajili vipimo vya nyuzijoto 48C huku wakaazi wa mji mkuu wa India New Delhi ukistahimili kiwango cha nyuzijoto 44C .
.
Maafisa wa utawala nchini humo wameanza kampeini ya kuwahamasisha wanainchi kukaa majumbani mwao na kuwashauri wanye waji mengi.
Yamkini viwango vya joto vimekuwa juu zaidi katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita lakini vifo vimeanza kuripotiwa mwishoni mwa juma.
Jimbo la Andhra Pradesh ndilo lililopoteza watu wengi zaidi ikiwa na jumla ya watu 246 waliopoteza maisha yao kuanzia juma lililopita.
Jimbo la Andhra Pradesh ndilo lililopoteza watu 
.
asilimia kubwa ya wale waliopoteza maisha ni watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 walioshinda nje ya majumba yao.'' alisema kamishna wa kupambana na majanga katika jimbo la Andhra Pradesh.
Wakfu wa waandishi wa habari wanasema kuwa watu 186 wameaga katika wilaya 10 za jimbo la Telangana.
Watu 58 wamekufa kuanzia siku ya jumamosi.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa imesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa hali hiyo ya joto kuendelea kwa siku kadha zijazo.
Wenyeji waamua kuakaa ndani na kuamua kunywa maji tu.
 .
Watu wengine kumi walpoteza maisha yao katika jimbo la Magharibi mwa Bengal.
Waendesha teksi ambazo hazina kiyoyozi hawataruhusiwa kuhudumu kwa saa tano katika mji mkuu wa Kolkata. Hii inafuatia vifo vya madereva wawili.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa inasema kuwa hali hiyo ya juu ya joto inatokana na ukosefu wa mvua.


WANAJESHI 7 WAUWAWA UKO TUNISIA.

WANAJESHI 7 WAUWAWA UKO TUNISIA.

.
Mwanajeshi mmoja nchini Tunisia amempigwa risasi na kuuawa baada ya kuwaua wenzake 7 .
Askari wengine 10 walijeruhiwa mmoja wao akiwa hali mahututi katika shambulizi lililotokea katika hafla ya kupeperusha bendera katika kambi ya kijeshi ya Bouchoucha.
Kwa mujibu wa msemaji wa idara ya ulinzi Belhassen Oueslati askari huyo alikuwa na matatizo ya kifamilia na kiakili.
Wakati wa tukio afisa huyo alikuwa amekatazwa kubeba silaha yeyote.
Duru zinasema kuwa askari huyo alimiminiwa risasi na kuuawa pia na wenzake, ili kumzima asiendelee kutekeleza maafa hayo kisha utulivu ukarejelewa.
Wakuu wamekanusha kuwa kisa hicho kilichofanyika katika kambi moja ya kijeshi mjini Tunis, sio ya kigaidi.
Lakini kilisababisha taharuki kubwa mjini humo, ambapo mnamo mwezi Machi, wapiganaji wa kiislamu waliokuwa na silaha waliwauwa zaidi ya watu 20, wengi wao watalii, baada ya kuvamia makavadhi ya Bardo mjini Tunis.
Bwana Ouselati alisema kuwa afisa huyo alimshambulia afisa mmoja kwa kisu kabla ya kumpokonya bunduki na kuitumia kuwashambulia maafisa wengine.
Aliongezea kusema kuwa ''ninahakika kuwa hilo lilikuwa tukio la kipekee wala sio la kigaidi''
MAGARI YAZIDI CHOMWA MOTO BURUNDI HALI BADO NI TETE.

MAGARI YAZIDI CHOMWA MOTO BURUNDI HALI BADO NI TETE.

.
Basi moja la uchukuzi limechomwa moto mjini Bujumbura Burundi na waandamanaji waliorejea mabarabarani kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Waandamanaji wanachoma moto magurudumu haswa katika eneo la Kanyosha.
Kitongoji hicho kimekuwa kitovu cha maandamano haya dhidi ya awamu ya tatu ya rais Nkurunziza.
.
Mwandishi wa BBC mjini Bujumbura Ismael Misigaro amesema milio ya risasi inasikika mjini humo.
Maandamano haya yanarejea baada ya kuuawa kwa kiongozi wa chama cha upinzani Zedi Feruzi nje ya nyumba yake katika mji mkuu Bujumbura.
Aidha wanaharakati wa upinzani nchini humo wamesitisha mazungumzo na serikali rais Pierre Nkurunziza ya kutaka kutanzua mzozo ulioko wa kisiasa.
Wandamanaji wakienderea na uchomaji matairi ya gari.
.
Mzozo huo unafuatia hatua ya Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Uamuzi ambao wengi wanasema kuwa unaenda kinyume na sheria na ndio iliyosababisha kuwepo kwa jaribio la kumpindua, na maandamano ya wiki kadhaa.
Tayari zaidi ya raia 100,000 wa taifa hilo wametorokea mataifa jirani.


PAPAFRANCIS: SIJATAZAMA TV KWA MIAKA 25.

PAPAFRANCIS: SIJATAZAMA TV KWA MIAKA 25.

.
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, amesema kuwa hajawahi kutazama runinga kwa miaka 25 sasa.
Papa Prancis ambaye amewatamausha wachanganuzi wa kanisa hilo kwa kususia maisha ya kifahari katika makao makuu ya kanisa Vatican alisema alitizama runinga mara ya mwisho tarehe 15 mwezi julai mwaka wa 1990.
Alikoma kutizama runinga baada ya kumuahidi maria mtakatifu kuwa angekoma kushiriki uraibu huo.

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, amesema kuwa hajawahi kutizama runinga kwa miaka 25 sasa                                                                                                                                                                            
Isitoshe raia huyo wa Argentina amesema kuwa hatumii mtandao wa intaneti.
Na akitaka kupata habari za kimataifa , Papa anasema kuwa huwa anatenga dakika 10 tu ya muda wake kusoma gazeti la kiitaliano.
Papa Francis vilevile anafuatilia habari za klabu yake maarufu huko Argentina kupitia kwa wahudumu       

Papa Francis vilevile anafuatilia habari za klabu yake maarufu huko Argentina kupitia kwa wahudumu wake ambao humsimulia yanayojiri.
Je unaweza kukaa mbali na Runinga yako Simu yako ama mtandao wa Intanet japo kwa siku moja ?


UFISADI WAWAWEKA HATIANI WABUNGE WANNE KENYA.

UFISADI WAWAWEKA HATIANI WABUNGE WANNE KENYA.



Kiongozi wa Mashtaka ametoa ruhusa ya kushtakiwa kwa mwaziri wanne  
Kutumia ujumbe kwa vyombo vya habari, mkuu wa mashtaka ya umma nchini Kenya Keriako Tobiko, hii leo amevumbua yaliyomo katika hati za kesi za mawaziri wanne.
Tume ya maadili na kupambana na ufisadi ya Kenya imependekeza waziri wa uchukuzi mMhandisi Michael Kamau na waziri wa leba Kazungu Kambi kushtakiwa na matumizi mabaya ya ofisi.
Mhandisi Michael Kamau anakumbwa na shutuma za kutumia fedha ubadhirifu wa fedha za umma na kufanya mabadiliko katika ubunifu wa barabara ambayo tiyari ilikuwa imetengenezwa na mashauri.
Kazungu Kambi naye anadaiwa keteuwa wanachama wawili katika bodi ya shirika la taifa la hazina ya uzeeni kinyume na sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari jana alasiri jumapili, afisa mkuu wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi Halakhe Waqo, alisema kwamba mawaziri wanne waliochunguzwa ni waziri wa Uchukuzi Mhandisi Michael Kamau, waziri wa ardhi, makao na ustawi wa miji bi Charity Ngilu, waziri wa kilimo Felix Kosgei, waziri wa leba Kazungu kambi, seneta wa Nairobi Mike Sonko na mbunge .
Tume hio imemwandikia rais Uhuru Kenyatta ombi la kuongeza muda wa uchunguzi wa kesi zilizobaki.
Siku sitini ambazo walikuwa wamepewa kukamilisha uchunguzi wa ripoti hiyo zimetimia leo.

Rais Uhuru Kenyatta alikuwa ametoa makataa ya siku 60 kushtakiwa kwa maafisa wakuu serikalini wafisadi
''Tumekuwa na shinikizo la kukamilisha kesi kwa wakati uliotolewa ila wajibu wetu wa kufanya uchunguzi wa kina ambao unaweza kustahimili uchunguzi mahakamani umetulazimu kuomba muda zaidi''alisema Halakhe Waqo
Kwa sasa tume hio imekamilisha kesi 56 kati ya 124 zilizowasilishwa kwa uchunguzi zaidi baada ya ripoti yao ya awali iliyokabidhiwa rais Kenyatta kuwasilishwa bungeni .
Kesi 21 tayari zimefikishwa kwa mkuu wa mashtaka ya umma Keriako Tobiko.
Kufikia sasa maafisa 19 wamefikishwa mahakamani na wengine 29, kulingana na afisa mkuu wa EACC, watafikishwa mahakamani siku chache zijazo katika maeneo kadhaa nchini yakiwemo Turkana, Machakos, Nyamira, Nairobi na Trans nzoia
Hata hivyo tume hii nayo pia imekumbwa na malumbano ya ndani kwa ndani ya shtuma za ufisadi, zilizosababisha kuchunguzwa kwa kiongozi wa tume hiyo na baadhi ya wanatume wake ambao hatimae walijiuzulu.

WAKATI WANANCHI WANAZIDI TESEKA MHE: NKURUNZINZA AMUA KUINGIA KIWANJANI KUSAKATA KABUMBU.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza ameendelea na burudani ya kucheza mpira mjini Bujumbura nchini humo.Huku maandamano ya raia kupinga kugombea kwake awamu ya tatu yakiendelea nchini .Polisi wamekua wakizuia maandamano hayo na kuuwawa baadhi ya raia.Hata hivyo rais huyo ameonekana kutojali akiendelea na mambo yake.
WASOMI WASEMA: JK AONA MBALI JUU YA MAMBO MENGI HAPA NCHINI

WASOMI WASEMA: JK AONA MBALI JUU YA MAMBO MENGI HAPA NCHINI


Akizungumza jana, Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu), Gaudence Mpangala alisema mwaka huu CCM itakuwa na ushindani mkali kuliko ilivyowahi kutokea kwenye uchaguzi wowote wa nyuma.
Wasomi na wachambuzi wa siasa wamesema Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ameona mbali kuwataka viongozi wa chama hicho kuteua mgombea wa urais anayekubalika ndani na nje ya chama wakisema bila kufanya hivyo wataangushwa na mgombea wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Akizungumza jana, Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu), Gaudence Mpangala alisema mwaka huu CCM itakuwa na ushindani mkali kuliko ilivyowahi kutokea kwenye uchaguzi wowote wa nyuma.
Alisema ushindani huo unatokana na kuwapo kwa mgombea urais wa Ukawa unaoundwa na vyama Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD.
“Vyama hivyo vimeamua kushirikiana kusimamisha mgombea mmoja kwenye nafasi ya urais, ubunge na udiwani, ushirikiano huo utatoa upinzani mkali kwa CCM,” alisema Mpangala.
Alisema CCM wameliona hilo na ndiyo maana Rais Kikwete ameona ni muhimu awaeleze wana CCM kwamba wanatakiwa kuchagua viongozi wanaokubalika na wananchi walio wengi, vinginevyo watashindwa.
“Yale mambo ya zamani ya kila kundi kuwa na mgombea wake yakirudiwa hivi sasa yatakigharimu chama hicho, wanatakiwa kuungana na kuweka mtu anayekubalika bila kujali makundi,” alisema.
Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Alexander Makulilo pia alisema Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utakuwa na tofauti kubwa na chaguzi zilizopita, hivyo lazima wapate mgombea maarufu.
Akitoa mfano wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 alisema: “Katika kipindi hicho Mkapa (Benjamin) hakuwa akifahamika sana ukilinganisha na wana-CCM wengine waliokuwa wakiwania nafasi hiyo lakini alishinda na kuwa rais. Mwaka huu wakijaribu kufanya hivyo wataanguka vibaya, hali ya kisiasa imebadilika,” alisema.
Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, viashiria vinaonyesha kuwa vyama vya upinzani vinazidi kuwa na nguvu mwaka hadi mwaka, akitaja Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita kama mfano... “Hata mgombea wa urais wa CCM, 2010 alipata kura chache ikilinganishwa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Hii ina maana vyama vya upinzani vinakua kwa kasi,” alisema.
Alisema kukithiri kwa rushwa na umaskini katika jamii kumewakatisha tamaa wananchi hivyo watahitaji kiongozi mwenye uwezo kupunguza matatizo hayo.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Dk Emmanuel Malya alisema Rais Kikwete anafahamu kuwa chama hicho kisipoweka wagombea wanaokubalika kitaanguka kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
“Kikwete ameliona hilo na wanachama wenzake wafahamu kuwa huu si wakati wa kuweka mtu wao, bali mtu anayekubalika na wananchi walio wengi,” alisema.

JWTZ YATOA SUPRISE KWA WANASONGEA BAADA YA KUPITISHA HAMSHA HAMSHA BILA WAO KUJUA

Chini ya  Brigedia Jenerali wa Kamandi ya Kusini, John Chacha

Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wilayani Songea jana limezua kizaa zaa kwa wananchi kufuatia kuvamia mitaani, maofisini (serikali na binafsi) makanisani na misikitini wakiwa na silaha huku magari yao yakiranda kila kona na kuanza upekuzi  kwa watu wote walokutana nao huku wakidai kuonyeshwa vitambulisho.
 
Aidha,indaiwa kuwa baadhi ya wakazi wa mjini hapo waliamua kujifungia ndani huku wengine wakisema kwamba jeshi hilo linawasaka  magaidi waliovamia katika mji wa Songea kutokana na jeshi hilo kutowafahamisha wananchi nini hasa dhumuni la msako huo.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela alipoulizwa alisema zoezi hilo ni la kawaida  huku akiwataka wakazi wa mjini songea  kuwa na amani na waendelee kufanya shughuli zao kama kawaida.
 
Naye  Brigedia Jenerali wa Kamandi ya Kusini, John Chacha alisema hiyo ni sehemu ya mafunzo kwa wanajeshi hao na kuongeza kuwa  jeshi hilo  hufanya mafunzo mbalimbali ya kujiimarisha ikiwamo ya kulinda miji, maporini na mengineyo.

CHUO CHA ZOOM POLYTECHNIC COLLAGE & DAN COMPUTER INSTITUTE


Wakufunzi wa chuo cha Zoom Polytechnic Collage & Dan Computer Institute wakiwa kwenye mahafari ya tatu 02/05/2015

Mwenyekiti wa chuo cha Zoom Polytechnic Collage & Dan Computer Institute akitoa neno kwa niaba ya wazazi 














WANACHUO WAKIWA NA MGENI RASIMI MBUNGE WA BUKOBA MJINI MWESHIMIWA HAMIS SUED KAGASHEKI NA HAMSHATZ.BLOGSPORT.COM GROUP LA MTU TATU (Hatibu,Mohamed & Shaidu)

 Wanachuo wakiwa katika Mahafari ya tatu Zoom Polytechnic Collage & Dan Computer Institute Bukoba Campus Wakiwa na Mgeni rasimi muheshimiwa Hamis Sued Kagasheki mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini akiwa amevalia joho la rangi tofauti na wahitimu wakimuelezea mgeni rasimi kuhusu somo la  NETWORKING linavyofanya kazi

 Wanachuo wakiwa katika Mahafari ya tatu Zoom Polytechnic Collage & Dan Computer Institute Bukoba Campus Wakiwa na Mgeni rasimi muheshimiwa Hamis Sued Kagasheki mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini akiwa amevalia joho la rangi tofauti na wahitimu wakimuelezea mgeni rasimi kuhusu somo la  NETWORKING linavyofanya kazi
 HAMSHATZ.BLOGSPORT.COM Group walivyokuwa wakionyesha Igizo lao katika Mahafari ya tatu tarehe 02/05/2015


HAMSHATZ.BLOGSPORT.COM Group walivyokuwa  katika Mahafari ya tatu tarehe 02/05/2015 (Mohamed .M. Tirubaza , HATIBU .K. OMARY wakiwa na mzazi wao

HAMSHATZ.BLOGSPORT.COM Group walivyokuwa wakionyesha Igizo katika Mahafari ya tatu tarehe 02/05/2015 (HATIBU .K. OMARY, Mohamed .M. Tirubaza  & Shahidu. A. Twaibu ) (means HAMSHA)

Hamshatz.blogsport.com wakiwa kwenye maojiano yanayohusu igizo lao

Hamshatz.blogsport.com wakiwa na marafiki wenzao katika kusherekea sherehe yao

Mr Mohamed .M. Tirubaza kushoto akiwa na rafiki yake Shahidu .A. Twaibu kulia wakiwa katika mahafari yao ya tatu tarehe 02/05/2015

HAMSHATZ.BLOGSPORT.COM Group walivyokuwa wakionyesha Igizo katika Mahafari ya tatu tarehe 02/05/2015 (HATIBU .K. OMARY, Mohamed .M. Tirubaza  & Shahidu. A. Twaibu ) (means HAMSHA)

Mr Mohamed .M. Tirubaza 

MAJAMBAZI SUGU WAKAMATWA MCHANA HUU JIJINI DAR WAKITAKA KUIBA BENKI YA NMB WASHUSHIWA VIPONDO NA WANANCHI PAMOJA NA MAPOLISI


MAJAMBAZI WAKAMATWA DAR


Wananchi wakiwa eneo la Benki ya NMB Sinza-Mori, Dar wakifuatilia tukio hilo.  POLISI jijini Dar wamewakamata watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa katika jaribio la kuiba pesa katika benki ya NMB iliyopo Sinza-Mori, Dar es Salaam. Tukio hilo limetokea mchana wa leo katika Benki ya NMB tawi la Sinza-Mori jijini Dar ambapo majambazi hao walikamatwa wakiwa katika harakati za kutekeleza tukio hilo. Majambazi hao baada ya kukamatwa wamepelekwa katika kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama jijini Dar

BASI LA WANAFUNZI LAGONGANA NA LORI LA MCHANGA


Haice ilivyokuwa ikionekana muda mfupi baada ya ajali
Lori la mchana likiwa limepinduka baada ya ajali



Ajali hiyo  imetokea leo jioni   eneo la Boma mbuzi pasua katika barabara iendayo kiwanda cha sukari TPC,imehusisha magari mawili ambayo ni Toyota haice yenye namba za usajili SU 37299 mali ya chuo cha mafunzo ya ufundi VETA lililogongana uso kwa uso na Tipa la mchanga lenye namba za usajili T 202 BFT na kusababisha tipa hilo kupinduka.
Kwa mujibu wa maelezo ya askari wa barabarani aliyefika katika eneo la tukio,aliyepata majeraha makubwa ni dereva (mwanafunzi) ambaye jina lake halijafahamika na amewahishwa kupata matibabu.



Kwa upande wa dereva wa lori hilo bwana Victor ambaye amepata mshituko katika mguu wake wa kulia ameelezea chanzo cha ajali hiyo kuwa ni dereva wa haice kuingia kwa kasi katika barabara hiyo akitokea upande wa kushoto wa barabara hiyo hivyo na kushindwa kulimudu gari na hatimaye kulifuata lori hilo.
Kushoto ni dereva wa Lori akiongea na askari wa barabarani ,aliyejishika kifuani ni mwalimu wa VETA aliyekuwa akiwaongoza wanafunzi katika haice iliyohusika katika ajali

Utingo wa lori akikusanya mchanga uliomwagika baada ya ajali
“Mimi nilikuwa nikipandisha kutokea upande wa Serengeti (breweries)   kwa kawaida nilitegemea derevawa haice angesubiri nipite kwani nilikuwa upande wake wa kulia lakini cha kushangaza aliingia bila kutoa ishara na gari ilipomshinda alikuja upande wangu,nilijaribu kumkwepa lakini ilishindikana kwani alisha karibia sana na baada ya kugongana gari langu lipinduka kutokana na uzito wa mchanga niliyokuwa nimebeba”.
Askari wa barabarani akijaribu kuwatuliza wananchi walitaka kumpiga mwalimu wa VETA
Hali ya tafrani ilizuka mara baada ya mwalimu wa VETA kumueleza askari wa usalama wa barabarani waliofika eneo hilo kuwa yeye pamoja na wanafunzi wake walikuwa wakitokea upande wa mjini jambo lililopingwa vikali na mashuhuda wa ajali hiyo kitendo kilichopelekea askari kuwatuliza wananchi hao ambao walitaka kumpiga mwalimu huyo.

Akizungumza na mwandishi wetu huku akiwa haoneshi ushirikiano wa kutosha mwalimu aliyekuwa akiwasimamia wanafunzi hao wa VETA (hakutaja jina) alieleza kuwa ndani ya haice kulikuwemo na wanafunzi ishirini akiwemo aliyejeruhiwa(dereva).
Askari wa barabarani wakifanya vipimo katika  ajali 

“Huyu mwalimu ndiyo mwenye makosa ,huwezi kumruhusu mwanafunzi aingize gari barabarani katika hali kama ile” alieleza bwana Hamis Mbwana mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo.
Wananchi waliokuwa wakishuhudia matukio yaliyojiri eneo la tukio

Hadi mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio gari maalum kwa ajili ya kuvuta na kuondoa magari hayo lilifika  ili kuruhusu shughuli nyingine za matumizi ya barabara kuendelea.

Kategori

Kategori