April 15, 2014, Muungano bado kasheshe
Kikao cha Bunge maalum la katiba kinaendelea leo hii, kinachojadiliwa hasa ni sura ya kwanza na sita ya Rasimu ya Katiba.
Kama ilivyo kawaida, wajumbe wanaendelea kulumbana, Chama Cha
Mapinduzi wakikazania Muundo wa serikali mbili na wale wa upinzani
wakitetea serikali tatu, kama ilivyowasilishwa na Tume Maalum ya
kukusanya maoni iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Wajumbe wa Bunge hilo kutoka Zanzibar, ambao ni muhimu sana kwa ajili
ya upatikanaji wa Katiba hii, kwa kuwa ni lazima theluthi mbili
wakubali ili kupitisha kipengele chochote, wanaendelea kuvutana, juu ya
serikali mbili au tatu huku pia wakipigana vijembe.
Zifuatazo ni baadhi ya kauli zilizosisimua kutoka kwa baadhi ya wajumbe
Mh. Mbaruku: Anaunga muundo wa serikali mbili maana ndiyo anaamini utawapa Zanzibar utajiri na Zanzibar itakuwa Half London.
Mh. Hija Hassan Hija:
Anasema watanganyika hawana hasara ya serikali mbili wala moja maana
walishachukua mali zote kwa miaka 50 iliyopita na Zanzibar wameibiwa kwa
miaka 50 iliyopita. Zanzibar ilipwe kwa muda huo.
Anasema wenye mali
ni Tanganyika, mawaziri wa Zanzibar wamekuwa wakisema muungano umekuwa
ukiwaonea na anashangaa ni nini kimewapata. Anasema kuna mawaziri wana
maslahi yao ndo maana wanashindwa kuipigania Zanzibar.
Anasema
hawatetei muungano bali wanatetea maslahi yao maana kuna watu walikuwa
wanapigania muungano ila baada ya kupewa uwaziri wakakaa kimya kwa hiyo
hawa ni wasaka tonge, wana njaa.
Mh. Pamela Masai: Anasema wajumbe wameacha maslahi yenye tija kwa watanzania wote na kukimbilia kwenye muundo wa serikali.
Anaunga mkono maoni ya wachache kwenye Kamati namba 10. Na anaunga mkono Lugha ya kiswahili kutumika kama lugha ya taifa.
Anapinga vipengele vya Uadilifu, uwajibikaji uwazi na usawa kuondoshwa kweye tunu ya taifa.
Anasema
kamati zote zimeunga mkono sura ya pili ibara ya sita 2(6), anasema kwa
hiyo hata mamlaka waliyonayo wajumbe wa BMK ni mamlaka waliyopewa
wananchi.
Anapendekeza muundo wa Serikali tatu. Anasema kama wananchi
wanataka serikali mbili basi waendelee na serikali tatu alafu wananchi
wapendekeze maoni ya muundo wa serikali wanayotaka.
Mh. Mwinyi Haji Makame: Anasema muungano huu waasisi wetu wameleta muungano wa undugu na sio vinginevyo.
Gari
ya serikali mbili ishachemka na haizuiliki, anasema hata wakina Jussa
wakileta unafiki na chuki muundo huu utaendelea kuwepo..
Anasema miaka 50 ya Mapinduzi ndiyo umeijenga Zanzibar.
Anamalizia
kwa kusema kuwa matatizo ya Zanzibar kwa muundo huu wa serikali mbili
yashashughulikiwa ndani ya kamati zote zilizoundwa kutatua matatizo ya
wazanzibar.
Mh. Chiku Abwao: Anaanza kwa kusema yeye ni muumini
wa muungano na muungano wa shirikisho ndiyo utaondoa muungano wa
manung'uniko na kuhakikisha Tanganyika inapatikana kwa gharama yoyote,
ananukuu ''Jasiri ni yule anayejali kwao''
Anasema bora muungano
uvunjike ila Tanganyika ibaki na anaunga muundo uliopendekezwa na tume
ya Warioba maana ni maoni ya wananchi walio wengi.
Anamnukuu Lukuvi
kuhusu jeshi kutawala nchi kama muundo wa serikali tatu ukipita na
kusema hata hivyo jeshi lipo kwa ajili ya wananchi wa Tanzania pia
anawasifu wazanzibar kwa kupigania utaifa wao.
Anasema wabunge walio
wengi wa tanzania hawapo bungeni kuunga muungano wa tanganyika na
zanzibar bali wapo kuunga mkono muungano wa TANU na AFRO-SHIRAZI Party.
Mh. Oluoch:
Anasema kumbe bungeni ni sehemu ambapo ukweli unaachwa na uongo
kuchukuliwa. Anasema hata waasisi waliunganisha mchanga wa Tanganyika na
Zanzibar ili kuunda serikali moja na sio mbili kama ilivyo sasa.
Anasema ikiwa wazanzibar wakitaka muungano hawatapiga kura ya kuunga muundo wa serikali mbili...
Anasema walimu wanaunga hoja serikali tatu.
Shamsa Mwangunga: Anatoa pongezi kwa serikali ya JMT kwa kulea muungano huu mpaka kufikia miaka 50 maana malezi yanapitia changamoto nyingi.
Anasema
muungano huu ni tunu maana nchi nyingi zimejaribu kuwa na muungano na
shirikisho ila hawakuweza kufika mbali ila kwa muungano huu wa Tanzania
ni suala la kujivunia kuwepo mpaka sasa hivi. Uvumilivu na upendo wa
watanzania ndo umeleta muungano huu kuwa imara na kero mbali mbali
zimeweza kutatuliwa na kubaki kero moja ya uchumi.
Utawala bora tumekuwa tukisifiwa duniani kwa kuwa na utawala bora kwa
kuweza kuudumisha muungano huu na kuna watu wamekuwa wakipotosha kuwa
kuna kero wakati sio kweli hakuna kero na kero zilizobaki ni ndogo na
zinafanyiwa kazi.
Anasema serikali ya nchi mbili ni zimwi tulijualo
na tumelizoe na serikali ya nchi tatu hatulijui ''Zimwi likujualo
halikuli likakwishaaaa''
Mh. Salehe Nassoro Juma:
Msimamo wake ni muungano wa serikali tatu na anawatoa wasiwasi
watanzania na wapemba wanaofanya biashara ya vitunguu tanzania bara kuwa
serikali tatu hazivunji muungano na kama ukivunjika tanzania imesaini
mkataka wa haki za binadamu na wataendelea kuishi kama DIASPORA hata
muungano ukivunjika.
Anamshukuru mh. Kikwete kwa kuanzisha mchakato
huu wa katiba mpya, maana kabla ya mchakato huu ilikuwa kosa la jinai
kuzungumzia muundo wa muungano.
Anasema hakuna asiyejua kuwa muundo
wa serikali mbili una tatizo na suluhisho la matatizo haya ni muundo wa
serikali tatu, anasema pia kuwa mawazo ya waasisi wetu yamezeeka inabidi
yafanyiwe modification na ametolea mfano wa China jinsi walivyofanyia
modification mawazo ya waasisi wao na mambo yanaenda vizuri.
Mh. Haji Omar:
Anaanza kwa kuunga mawazo aliyoyatoa kwenye kamati no 7 mawazo ya walio
wengi kwenye sura ya 1 & 6 juu ya muundo wa serikali mbili.
Uhalai
wa Karume kuchukua dhamana ya watu wa Zanzibar kuhusu muungano, anasema
mzee Karume alikuwa anatimiza ilani ya chama chake cha ASP juu ya umoja
na kuhakikisha elimu, matibabu yanakuwa bure na makazi bora kwa
wazanzibar wote.
Faida za muungano, anasema
1.Umeme jimbo la Tumbatu
2. -Anasema wananchi walio wengi Zanzibar wanaunga muundo wa serikali mbili.
Mh. Ezekiel Maige:
Anasema kuwa lugha zinazotolewa na Wazanzibari zina ukakasi. Anasema
kuwa Zanzibar ina wilaya 10 ambazo zote zina barabara za lami na umeme
tofauti na Tanzania Bara.
Anasema kuwa hayo yote hawayaoni na badala
yake wanazidi kulalamika kuwa wanaonewa na Bara. Anahoji iwapo ikatokea
Zanzibar kukawa na utajiri mkubwa kuliko Bara, je Wazanzibari watakuwa
tayari kuisaidia Bara?
Mh. Fahmi Dovutwa: Alama
za taifa zitakua wimbo wa taifa, nembo ya taifa na bendera. Dola
haimtambui Mungu kwa hiyo wimbo wa taifa itolewe kwenye alama ya taifa.
dhana ya kuomba Mungu asaidie ina maana dola haifungamani na dini. Nami
ntasimama nitapigana kuhakikisha Katiba inamtambua Mungu.
Kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine. Sera ya TANU iliruhusu wazee
watoto na walemavu kunyonya. Nataka iwe kutegemeana sio kunyonyana.
Watu wanaoamini serikali tatu mpaka sasa wameshindwa kutuonesha jinsi
watakavyotatua matatizo tulio nayo. watu wa serikali tatu wameshindwa
kujenga hoja. Namlaumu sana Mbowe. Chadema wana serikali za majimbo
lakini wanashindwa kufafanua vizuri.
Natoa shukrani za pekee za Rais kwa kuridhia hii ijadiliwe na kusimamia elimu za kata. Namshukuru pia Lowasa aliye mshauri Rais.
Mh. Joseph Mbilinyi: Naunga mkono serikali tatu kama ilivyoletwa na Tume ya katiba, kwa hiyo tunaunga mkono maoni ya wananchi.
Aliyeharibu huu mchakato ni Rais aliyekuja kuelezea msimamo wa chama chake badala ya kuzindua bunge.
Hiki ni kipindi cha Kwaresma acheni unafiki. Tumeharibu pesa nyingi.
CCM wameishiwa mikakati wameanzisha mkakati wa kuzomea. Mwingulu anataka
serikali moja lakini anaogopa kusema. Tuko kwenye nafasi nzuri sana la
kujadili hili suala la sivyo tutalijadili kwa kulazimishwa.
Leo
Lukuvi anatutishia nchi itatawaliwa na jeshi, vizuri, mbona Rais wetu
alikua mwanajeshi na anatuongoza? wanajeshi ni ndugu zetu, wakitawala
kuna tatizo gani?
Serikali tatu ni tija. kila
chenye gharama kina faida. Mara nyingi viongozi wa dini wanakosea
wanapokuwa upande wa dola dhidi ya wananchi. Mfano Rwanda. Unapopima
malaria au ukimwi inapimwa kwenye kidole sio mwili mzima acheni kuzingua
eti waliohojiwa ni wachache.