hamshatz.blogsport.com
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amejitokeza kwa mara ya kwanza tangu jaribio la mapinduzi la jumatano iliyopita.
Rais
Nkurunziza akihutubia waandishi wa habari katika ikulu ya Bujumbura
alionya kuwa kuna tishio la shambulizi la kigaidi kutoka kwa kundi la
waislamu kutoka Somalia wenye uhusiano na Al-Qaeda , Al Shabaab.
Aliwaambia wandishi wa habari wa kimataifa kuwa tishio hilo la mashambulizi sio tu kwa taifa lake bali pia kwa Kenya na Uganda .
Hata
hivyo mwaandishi wa BBC aliyeko Bujumbura anasema kuwa Nkurunziza
hakuzungumzia lolote kuhusu hali ilivyo nchini Burundi wala tishio la
mapinduzi dhidi yake.
Wapinzani wake wanashuku ni njama ya kuidhinisha makabiliano makali na waandamani hapo kesho
Aliondoka ghafla akiwa mongoni mwa msafara uliolindwa kikamilifu.
Wapinzani
wake hata hivyo wanasema huenda hiyo ni njama ya rais Nkurunziza
kuidhinisha makabiliano makali dhidi ya wapinzani wake ambao tayari
wameagiza wafuasi wao kujitokeza kwa wingi hapo kesho kuendelea na
maandamano ya kumtaka asiwanie kipindi cha tatu katika kura za urais
zitakazofanyika mwezi ujao.
Al Shabab wametishia kuishambulia Burundi kufuatia mchango wake katika majeshi ya AMISOM
Duru
kutoka kwa afisi za maswala ya usalama wanje katika serikali ya
Marekani na vile vile maswala ya ndani ya serikali ya Uingereza
zimekariri tishio hilo la Al Shaabab dhidi ya Burundi kufuatia mchango
wake katika jeshi la umoja wa Afrika Amisom huko Somalia.
Marekani
tayari imeagiza raia wake kuondoka nchini humo kufuatia tishio la
shambulizi la kigaidi mbali na kuzorota kwa hali ya usalama
Hamsha+255
SIASA
RAIS NKURUNZIZA AONGEA NA WAANDISHI KWA MARA YA KWANZA NA KUWATOLEA UVIVU AL-SHABAAB BAADA YA KUFELI KWA JARIBIO LA KUMPINDUA BURUNDI.