KUKUA KWA TEKNOLOJIA SASA KUNA VIATU VINAVYOJIFUNGA KAMBA



Nike-Mag-Sneakers.

Kadri siku zinavyozidi kwenda Teknolojia nayo imezidi kutupeleka mbali, mengi yanatushangaza na kwa hali ilivyo mengine ya kutushangaza hayako mbali pia kuja!
 
Ni kama miaka 20 imepita  tangu tuone viatu vikijifunga kamba kwenye matangazo ya viatu, majibu yakawa rahisi, utaalamu wa Kompyuta ulifanikisha kutengeneza matangazo ya namna hiyo, 2015 Kampuni ya Nike imeamua kufanya kweli.
 
Wataalamu Ujerumani wamefanikiwa kubuni viatu ambavyo vina uwezo wa kujifunga kamba vyenyewe,  unapovaa kiatu hicho, sensa ya kiatu inaamrisha zinajifunga zenyewe baada ya mguu kukawa sawa.
 
24B4B70800000578-2910706-image-a-17_1421283782293 
 
Kali zaidi ni pale unapotaka kuvua viatu utahitajika kubonyeza au kugonga visigino vya kiatu mara mbili na kisha kamba za viatu zinafunguka, kiatu hicho hakihitaji kuwekwa kwenye charger au kubadilishwa betri, mvaaji anapozidi kutembea ndipo anapozidi kukiongezea nguvu.

24B4B70400000578-2910706-The_German_scientists_used_an_energy_harvester_attached_to_the_s-a-32_1421285653813 (1).
 
F0FDQE6GB3W26UH.MEDIUM 
 
Nike 
 
download (2)