NITAONDOKA TUWESTHAM:SAM ALLARDYCE AFUNGUKA

.
Kocha wa timu ya soka ya West Ham United ya England Sam Allardyce amefichua mpango wake wa kuondoka klabuni hapo hata kama timu hiyo ilimpa nafasi ya mkataba mpya.
Taarifa za kuondoka kwa Allardyce zilitangazwa dakika za mwisho za mechi kati ya West Ham dhidi ya Newcastle United, mtanange ambao uliisha kwa ushindi wa bao mbili kwa bila walioupata Newcastle na kujinasua katika janga la kushuka daraja. Allardyce ametumia miaka minne kuifundisha West Ham lakini wagonga nyundo hao wameamua kutompa tena mkataba mpya katika majira haya ya joto. "sikutaka kubaki, naweza sema kama tulikuwa tunafikra sawa kama na wao hawakuwa wenye kunihitaji pia" alisema Kocha huyo.