Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo SPORTS. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo SPORTS. Onyesha machapisho yote
NITAONDOKA TUWESTHAM:SAM ALLARDYCE AFUNGUKA

NITAONDOKA TUWESTHAM:SAM ALLARDYCE AFUNGUKA

.
Kocha wa timu ya soka ya West Ham United ya England Sam Allardyce amefichua mpango wake wa kuondoka klabuni hapo hata kama timu hiyo ilimpa nafasi ya mkataba mpya.
Taarifa za kuondoka kwa Allardyce zilitangazwa dakika za mwisho za mechi kati ya West Ham dhidi ya Newcastle United, mtanange ambao uliisha kwa ushindi wa bao mbili kwa bila walioupata Newcastle na kujinasua katika janga la kushuka daraja. Allardyce ametumia miaka minne kuifundisha West Ham lakini wagonga nyundo hao wameamua kutompa tena mkataba mpya katika majira haya ya joto. "sikutaka kubaki, naweza sema kama tulikuwa tunafikra sawa kama na wao hawakuwa wenye kunihitaji pia" alisema Kocha huyo.
REALMADRID YAMTIMUWA CARLO ANCELOTTI

REALMADRID YAMTIMUWA CARLO ANCELOTTI

.
Hatimaye miamba ya soka nchini Hispania Real Madrid imemtimua kocha wa timu hiyo Carlo Ancelotti baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa misimu miwili.
Kocha huyo raia wa Italia, aliiongoza Madrid kutwaa taji la kombe la Hispania kabla ya kuibebesha miamba hiyo taji la kumi la klabu bingwa barani Ulaya. Pamoja na mafanikio hayo aliyoyapata msimu uliopita, mwaka huu haukuwa mzuri kwa vijana hao wa Benabeu baada ya kuambulia patupu kwa kukosa hata kombe moja japokuwa kikosi cha timu hiyo kinatajwa kuwa cha gharama ya juu. Hasira za viongozi wa klabu hiyo ziliongezeka baada ya kutupwa nje na Juventus katika hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya huku wapinzani wao wakubwa Barcelona ikinyakuwa taji la ligi kuu na kutinga fainali ya klabu bingwa na kombe la Hispania. Rais wa Madrid Florentino Perez amewaambia waandishi wa habari kuwa haikuwa rahis kumtema kocha huyo na kuongeza kuwa kocha mpya atateuliwa wiki ijayo.

WAKATI WANANCHI WANAZIDI TESEKA MHE: NKURUNZINZA AMUA KUINGIA KIWANJANI KUSAKATA KABUMBU.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza ameendelea na burudani ya kucheza mpira mjini Bujumbura nchini humo.Huku maandamano ya raia kupinga kugombea kwake awamu ya tatu yakiendelea nchini .Polisi wamekua wakizuia maandamano hayo na kuuwawa baadhi ya raia.Hata hivyo rais huyo ameonekana kutojali akiendelea na mambo yake.
DROGBA AIAGA CHELSEA UKU MASHABIKI WAKIMSHANGILIA

DROGBA AIAGA CHELSEA UKU MASHABIKI WAKIMSHANGILIA

Kategori

Kategori