Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, amesema kuwa hajawahi kutazama runinga kwa miaka 25 sasa.
Papa
Prancis ambaye amewatamausha wachanganuzi wa kanisa hilo kwa kususia
maisha ya kifahari katika makao makuu ya kanisa Vatican alisema
alitizama runinga mara ya mwisho tarehe 15 mwezi julai mwaka wa 1990.Alikoma kutizama runinga baada ya kumuahidi maria mtakatifu kuwa angekoma kushiriki uraibu huo.
Na akitaka kupata habari za kimataifa , Papa anasema kuwa huwa anatenga dakika 10 tu ya muda wake kusoma gazeti la kiitaliano.
Papa Francis vilevile anafuatilia habari za klabu yake maarufu huko Argentina kupitia kwa wahudumu wake ambao humsimulia yanayojiri.
Je unaweza kukaa mbali na Runinga yako Simu yako ama mtandao wa Intanet japo kwa siku moja ?