MAJAMBAZI SUGU WAKAMATWA MCHANA HUU JIJINI DAR WAKITAKA KUIBA BENKI YA NMB WASHUSHIWA VIPONDO NA WANANCHI PAMOJA NA MAPOLISI
MAJAMBAZI WAKAMATWA DAR
Wananchi wakiwa eneo la Benki ya NMB Sinza-Mori, Dar wakifuatilia tukio hilo. POLISI jijini Dar wamewakamata watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa katika jaribio la kuiba pesa katika benki ya NMB iliyopo Sinza-Mori, Dar es Salaam. Tukio hilo limetokea mchana wa leo katika Benki ya NMB tawi la Sinza-Mori jijini Dar ambapo majambazi hao walikamatwa wakiwa katika harakati za kutekeleza tukio hilo. Majambazi hao baada ya kukamatwa wamepelekwa katika kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama jijini Dar