Haice ilivyokuwa ikionekana muda mfupi baada ya ajali |
Lori la mchana likiwa limepinduka baada ya ajali |
Ajali hiyo imetokea leo jioni eneo la Boma mbuzi pasua katika
barabara iendayo kiwanda cha sukari TPC,imehusisha magari mawili ambayo
ni Toyota haice yenye namba za usajili SU 37299 mali ya chuo cha mafunzo
ya ufundi VETA lililogongana uso kwa uso na Tipa la mchanga lenye namba
za usajili T 202 BFT na kusababisha tipa hilo kupinduka.
Kwa mujibu wa maelezo ya askari wa barabarani aliyefika katika eneo la
tukio,aliyepata majeraha makubwa ni dereva (mwanafunzi) ambaye jina lake
halijafahamika na amewahishwa kupata matibabu.
Kwa upande wa dereva wa lori hilo bwana Victor ambaye amepata mshituko
katika mguu wake wa kulia ameelezea chanzo cha ajali hiyo kuwa ni dereva
wa haice kuingia kwa kasi katika barabara hiyo akitokea upande wa
kushoto wa barabara hiyo hivyo na kushindwa kulimudu gari na hatimaye
kulifuata lori hilo.
Kushoto ni dereva wa Lori akiongea na askari wa barabarani ,aliyejishika kifuani ni mwalimu wa VETA aliyekuwa akiwaongoza wanafunzi katika haice iliyohusika katika ajali |
Utingo wa lori akikusanya mchanga uliomwagika baada ya ajali |
Askari wa barabarani akijaribu kuwatuliza wananchi walitaka kumpiga mwalimu wa VETA |
Akizungumza na mwandishi wetu huku akiwa haoneshi ushirikiano wa kutosha mwalimu aliyekuwa akiwasimamia wanafunzi hao wa VETA (hakutaja jina) alieleza kuwa ndani ya haice kulikuwemo na wanafunzi ishirini akiwemo aliyejeruhiwa(dereva).
“Huyu mwalimu ndiyo mwenye makosa ,huwezi kumruhusu mwanafunzi aingize
gari barabarani katika hali kama ile” alieleza bwana Hamis Mbwana mmoja
wa mashuhuda wa ajali hiyo.