Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo SPORTS. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo SPORTS. Onyesha machapisho yote
NITAONDOKA TUWESTHAM:SAM ALLARDYCE AFUNGUKA

NITAONDOKA TUWESTHAM:SAM ALLARDYCE AFUNGUKA

.
Kocha wa timu ya soka ya West Ham United ya England Sam Allardyce amefichua mpango wake wa kuondoka klabuni hapo hata kama timu hiyo ilimpa nafasi ya mkataba mpya.
Taarifa za kuondoka kwa Allardyce zilitangazwa dakika za mwisho za mechi kati ya West Ham dhidi ya Newcastle United, mtanange ambao uliisha kwa ushindi wa bao mbili kwa bila walioupata Newcastle na kujinasua katika janga la kushuka daraja. Allardyce ametumia miaka minne kuifundisha West Ham lakini wagonga nyundo hao wameamua kutompa tena mkataba mpya katika majira haya ya joto. "sikutaka kubaki, naweza sema kama tulikuwa tunafikra sawa kama na wao hawakuwa wenye kunihitaji pia" alisema Kocha huyo.
REALMADRID YAMTIMUWA CARLO ANCELOTTI

REALMADRID YAMTIMUWA CARLO ANCELOTTI

.
Hatimaye miamba ya soka nchini Hispania Real Madrid imemtimua kocha wa timu hiyo Carlo Ancelotti baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa misimu miwili.
Kocha huyo raia wa Italia, aliiongoza Madrid kutwaa taji la kombe la Hispania kabla ya kuibebesha miamba hiyo taji la kumi la klabu bingwa barani Ulaya. Pamoja na mafanikio hayo aliyoyapata msimu uliopita, mwaka huu haukuwa mzuri kwa vijana hao wa Benabeu baada ya kuambulia patupu kwa kukosa hata kombe moja japokuwa kikosi cha timu hiyo kinatajwa kuwa cha gharama ya juu. Hasira za viongozi wa klabu hiyo ziliongezeka baada ya kutupwa nje na Juventus katika hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya huku wapinzani wao wakubwa Barcelona ikinyakuwa taji la ligi kuu na kutinga fainali ya klabu bingwa na kombe la Hispania. Rais wa Madrid Florentino Perez amewaambia waandishi wa habari kuwa haikuwa rahis kumtema kocha huyo na kuongeza kuwa kocha mpya atateuliwa wiki ijayo.

WAKATI WANANCHI WANAZIDI TESEKA MHE: NKURUNZINZA AMUA KUINGIA KIWANJANI KUSAKATA KABUMBU.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza ameendelea na burudani ya kucheza mpira mjini Bujumbura nchini humo.Huku maandamano ya raia kupinga kugombea kwake awamu ya tatu yakiendelea nchini .Polisi wamekua wakizuia maandamano hayo na kuuwawa baadhi ya raia.Hata hivyo rais huyo ameonekana kutojali akiendelea na mambo yake.
DROGBA AIAGA CHELSEA UKU MASHABIKI WAKIMSHANGILIA

DROGBA AIAGA CHELSEA UKU MASHABIKI WAKIMSHANGILIA

STARS KUWAVAA SWAZILAND ROYAL BAFOKENG

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza mchezo wake wa kwanza  wa kombe la COSAFA siku ya jumatatu dhidi ya Swaziland katika uwanja wa Royal Bafokeng pembeni kidogo ya jiji la Rustenburg kuanzia majira ya saa 1:30 jioni kwa saa za Afrika Kusini.

Awali michezo ya kundi B ilikuwa ifanyike katika uwanja wa Olympia Park, lakini waandaji wa michuano ya COSAFA Castle wamesema kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wao michezo hiyo imeshindikana kufanyika katika uwanja huo.

Uwanja wa Royal Bafokeng ni miongoni mwa viwanja viliyotumika katika Fainali za Kombe la Dunia 2010 chini Afrika kusini, ukiwa na uwezo wa kubeba watazamaji  42,000 huku timu ya Platinum Stars iliyopo Ligi Kuu ikiutumia kama uwanja wake wa nyumbani.
Leo asubuhi Taifa Stars imefanya mazoezi katika uwanja wa shule ya Rustenburg chini ya kocha mkuu Mart Nooij, na wachezaji wote wapo katika hali nzuri kuelekea katika mchezo huo wa jumatatu.


Kesho jioni Taifa Stars ifanya mazoezi saa jioni katika uwanja wa Rolay Bafokeng kwa ajili ya kuuzoea uwanja kabla ya mchezo wenyewe dhidi ya Swaziland.

Akiongelea hali ya hewa, kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij amesema vijana wake wanaendelea kuizoea hali ya hewa, japokuwa kuna baridi hakuna mchezaji aliyeshindwa kufanya mazoezi kutokana na hali ya hewa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Mgomo ligi kuu Hispania .

Mgomo ligi kuu Hispania .

Barcelona's Lionel Messi from Argentina, centre left, scores his goal during a Spanish La Liga soccer match between Real Madrid and FC Barcelona at the Santiago Bernabeu  stadium in Madrid, Spain, Sunday, March 23, 2014. (AP Photo/Andres Kudacki)

Barcelona's Lionel Messi from Argentina, centre left, scores his goal during a Spanish La Liga soccer match between Real Madrid and FC Barcelona at the Santiago Bernabeu  stadium in Madrid, Spain, Sunday, March 23, 2014. (AP Photo/Andres Kudacki)
Barcelona’s Lionel Messi from Argentina, centre left, scores his goal during a Spanish La Liga soccer match between Real Madrid and FC Barcelona at the Santiago Bernabeu stadium in Madrid, Spain, Sunday, March 23, 2014. (AP Photo/Andres Kudacki)

Klabu za ligi kuu nchini Hispania zinatarajiwa kufanya mgomo mwishoni mwa wiki hii ambapo hakutakuwa na michezo yoyote kufuatia kushindwa kupatikana kwa makubaliano katika mkutano uliofanyika kati ya shirikisho la wachezaji , uongozi wa ligi pamoja na shirikisho la soka la Hispania .
Mgomo huu unakuja baada ya taarifa toka Serikalini ambayo iliarifu juu ya kuwepo kwa makubaliano mapya ya mikataba ya televisheni ambapo timu zote 20 zitaweza kufanya makubaliano ya mkataba wa haki za matangazo ya televisheni kwa umoja na sio tofauti na klabu kubwa za Real Madrid na Barcelona .
Umoja wa wachezaji unahisi kuwa bado matatizo yanayohusu malipo na haki zao hayajapewa kipaumbele na hivyo kwa kauli moja wamekubaliana kufanya mgomo ambao kimsingi utavuruga ratiba ya ligi ya Hispania .
Rais wa umoja wa wachezaji AFE Luis Rabes amethibitisha kuwa hakuna muafaka uliofikiwa na pande zote katika kikao kilichofanyika hii leo (jumanne) na kwa jinsi hali ilivyo hakutakuw ana michezo ya ligi ya Hispania wikiendi hii .
Hata hivyo bado kuna nafasi ya hali hii kubadilika kwani pande zote zinazohusika kwenye mazungumzo haya zitakutana katika mazungumzo mengine hapo kesho na endapo muafaka utafikiwa basi huenda michezo ya mzunguko wa 37 ikaendelea .
Hadi sasa Fc Barcelona ndio wanaongoza ligi na watajihakikishai kutwaa ubingwa endapo watashinda mchezo wao dhidi ya Atletico Madrid siku ya jumapili huku wakiwaacha mabingwa watetezi Atletico Madrid wakishindwa kutetea ubingwa wao .
Suarez Kuikosa Copa America.

Suarez Kuikosa Copa America.

cms-image-000008168

Mshambuliaji nyota wa timu ya Barcelona Luis Suarez atakuwa nje ya michuano ya mataifa ya Amerika ya kusini maarufu kama Copa America kutokana na kuendelea kutumikia adhabu ya kukosa michezo tisa kufuatia kosa la kumng’ata beki wa Italia Giorgio Chielini kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka jana .

Suarez atalazimika kuwatazama wenzie kwenye televisheni kutokana na adhabu hiyo ambayo imebakiza michezo saba kabla ya kumalizika .

Uruguay inayofundishwa na kocha mkongwe Oscar Washington Tabarez italazimika kumtegemea mshambuliaji wa PSG Edinson Cavani kwenye idara ya ushambuliaji huku ikimkosa pia Diego Forlan ambaye amestaafu kucheza timu ya taifa .

Forlan ambaye alistaafu mwezi machi mwaka huu amesema kuwa anaamini Uruguay ina wachezaji wazuri na wenye uwezo ambao wataziba pengo la Suarez na kufanya vizuri kwenye michuano ya mwaka huu .

Uruguay ndio mabingwa watetezi wa michuano ya Copa America ambayo waliitwaa mwaka 2011 nchini Argentina ambako waliwafunga Paraguay kwenye fainali na wanaingia kwenye michuano ya mwaka huu kama moja ya timu zinazopewa nafasi ya kufanya vizuri
SIMULIZI YA MAJONZI KUTOKA KWA EMMANUEL ADEBAYOR YAVUTA HISIA ZA WENGI

SIMULIZI YA MAJONZI KUTOKA KWA EMMANUEL ADEBAYOR YAVUTA HISIA ZA WENGI



Miezi michache tu baada ya kumlaumu mamake mzazi kwa kumroga na kumfanya apoteze fomu yake, Emmanuel Adebayor anayeichezea timu ya Tottenham inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza, amejitokeza na kufichua jinsi familia yake ilivyomfanya afilisike bila shukrani.
Kupitia ukurasa wake wa facebook, Adebayor ameeleza kuwa

"Nimekuwa nikiziweka taarifa hizi kwa muda mrefu lakini leo nimehisi kuwa ni muhimu kuwaeleza nanyi pia. Ni kweli kuwa masuala ya familia hayastahili kuwekwa hadharani lakini nafanya hivi ili familia nyingine nazo zipate funzo kupita yaliyonisibu, Aliandika.
Anasema wakati alipokuwa na umri wa miaka 17, aliutumia mshahara wake wa kwanza kuijengea familia yake nyumba.Kama mnavyojua nilipokea tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika wa mwaka, mwaka 2008.

Nilimpandisha mama yangu jukwaani kumshukuru yeye kwa mambo yote. Mwaka ule ule nilimleta London kwa ajili uchunguzi wa afya yake.
Wakati binti yangu alipozaliwa niliwasiliana na mama yangu kumweleza lakini alikata simu na sikujua ni kwanini.

Ukisoma maoni yangu ya hivi karibuni watu wanasema mimi na familia yangu twende tupate ushauri kwa muhubiri maarufu wa dini ya kikristo T.B Joshua.

Mwaka 2013 nilimpa mama yangu pesa ili aende kupata ushauri kwa mhubiri huyo nchini Nigeria.
Alipaswa kukaa huko kwa wiki moja, lakini siku mbili tu alipofika nilipokea simu kwamba ameondoka. Zaidi ya hayo nilimpa mama yangu pesa nyingi kuanzisha biashara ya kupika chakula pamoja na bidhaa nyingine.
Kiuhalisia niliwaruhusu kuweka jina langu na picha yangu kwenye biashara hiyo ili waweze kuvutia wateja.
Ni kitu gani kingine mtoto wa kiume anaweza kufanya ndani ya uwezo wake kusaidia familia yake?
Miaka kadhaa iliyopita, nilinunua nyumba huko East Lagon nchini Ghana kwa dola milioni 1.2 za kimarekani. Nikaona ni vyema dada yangu mkubwa Yabo Adebayor kuishi katika nyumba hiyo. Vile vile nilimruhusu kaka yangu Daniel naye aishi kwenye nyumba hiyo.

Miezi michache baadae nilifukuzwa kwenye nyumba niliyokuwa naishi ikianibidi kwenye hiyo nyumba yangu. Kilichonishangaza niliona magari mengi kwenye barabara. Kwa kweli dada yangu aliamua kuikodisha hiyo nyumba pasipo kunieleza. Alimfukuza Daniel kwenye hiyo nyumba.

Mfahamu kwamba nyumba hiyo ina vyumba 15. Nilipompigia dada yangu anipe ufafanuzi alichukua karibu nusu saa kunishambulia na kunitukana kwenye simu. Nilimpigia mama yangu anaelezee kisa kizima naye akafanya kama dada yangu alivyofanya. Hivyo ni kama dada yangu alivyosema sina shukrani.

Kaka yangu Kola Adebayor, anaishi nchini Ujerumani kwa miaka ishirini na mitano sasa,safari zake zote za kurejea nyumbani mara nne ametumia gharama zangu,kama hiyo haitoshi ninawasomesha watoto wake na kuwalipia gharama zote kuhusiana na elimu yao.

Nilipokuwa nchini Monaco ,alinifuata na kutaka pesa za kuanzishia biashra yake .Mungu pekee ndiye ajuaye nilimpa kiasi gani cha kufungulia biashara yake,kama ukimuuliza biashara hiyo iko wapi leo?
Masahibu hayakuishia hapo,kaka yetu Peter alipoaga dunia nilimtumia Kola kiasi kikubwa cha pesa ili arejee nyumbani,cha kushangaza hakutokea msibani ama siku ya maziko.na leo kaka yule yule (Kola) anawaambia watu kuwa chanzo cha kifo cha kaka yetu Peter ni mimi,linawezekanaje hili? Kaka huyu huyu alikwenda kwenye gazeti la"The Sun" na kueleza habari za uongo kuhusiana na familia yetu ili kujipatia fedha.

Wakatuma barua pia katika klabu ya mpira ya Madrid nikafukuzwa.nilipokuwa nchini humo pia nilipata wazo kuwa ni vyema kuwa na familia ya wana soka,hivyo nikahakikisha kaka yangu Rotimi anajiunga na chuo cha mafunzo ya mpira huko Ufaransa. Miezi michache tu,wachezaji ishirini na saba wa chuo hiyo aliwaibia simu za mkononi wachezaji ishirini na mmoja .Sikuongea chochote kuhusiana na kaka Peter Adebayor ,kwasababu hayuko nasi leo hii,Mungu ailaze mahala pema peponi ,amina.

Dada yangu sasa, Lucia Adebayor amekuwa na tabia ya kuwaambia watu kuwa baba yetu amenitaka nimchukue dada huyu na kumpeleka ulaya,lakini sababu kubwa hasa ni nini ya kumpeleka huko ulaya? Kila aliyeko hapa yupo kwa sababu.

Nilirejea nyumbani Ghana nilipata taarifa za kaka yangu anaumwa sana,niliendesha gari kwa kasi sana kuelekea Togo ili kukutana naye na kumpa msaada anaostahili,nilipowasili huko mama yangu akanikatalia kumwona na kunieleza kuwa ninachopaswa kufanya ni kumpa mama yangu pesa nay eye ata maliza kila kitu.

Mungu pekee ndiye ajuaye siku ile ile nikampatia mama yangu kiasi cha pesa alichokitaka,lakini cha ajabu watu wanalalama kuwa sikufanya lolote kuokoa maisha ya kaka yangu Peter.je mimi ni mpumbavu kiasi gani niendeshe gari mpaka Togo bure bila ya sababu?

Nikaandaa mkutano wa kifamilia mwaka 2005 ili tumalize tofauti zetu na matatizo yanayotuzunguuka.nilipowauliza maoni yao wakanitaka kuwajengea nyumba kila mmoja wao na mishahara mikubwa kila mwezi kwa kila mmoja wao.

Leo hii niko hai wamejimilikisha kila kilicho change je nikifa itakuwaje?kwa sababu zote hizi,itanichukua muda mrefu mno kuweka mikakati na misingi yangu barani Africa.kila wakati ninajitahidi kuwasaidia wahitaji,familia yangu wao huhoji kila nifanyacho na wote huona nimefanya uamuzi mbaya.

Ikiwa leo ninaandika haya,sina lengo la kuwaanika watu wa familia yangu.ninataka familia zingine za kiafrika kujifunza kutokana na ninayoyapitia mimi. Asanteni sana

Kategori

Kategori