Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na
Mbunge wa zamani wa Kahama James Lembeli ambaye ni mwanachama wa
Chadema mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano mjini Kahama mkoani
Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John
Pombe Magufuli akimpongeza Mbunge wa zamani wa Kahama James Lembeli mara
baada ya kuwasalimia wananchi waliofika kwa ajili ya kumsikiliza Rais
katika viwanja hivyo vya Kahama. Wakati jana Rais Magufuli akiwa
wilayani Kahama mkoani Shinyanga alimpa nafasi aliyekuwa Mbunge wa
Kahama kwa tiketi ya CCM na baadae kuhamia CHADEMA, James Lembeli ili
azungumze.
Lembeli aliongea mambo kadhaa ikiwemo
hatma yake kurudi CCM ambapo alisema yupo tayari kurudi iwapo Rais
Magufuli atakisafisha chama kwa kuwashughulikia wanafiki na wala rushwa Hapa chini ni maneno ya James Lembeli katika mkutano huo.
ALIYEKUWA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela, (Pichani) ameibukia
kanisani na kutoa ya moyoni, ikiwa siku tano baada ya Rais Dk. John
Magufuli kutengua uteuzi wake.
Kilango, ambaye Jumatatu wiki hii
uteuzi wake ulitenguliwa baada ya Machi 20, mwaka huu, kudai kuwa mkoa
wa Shinyanga hauna mtumishi hewa wa serikali hata mmoja.
Hata
hivyo, Ikulu ilifanya uchunguzi na kubaini kuwa katika taarifa za awali
kuna watumishi hewa 45, huku kazi ya uhakiki ikiendelea katika wilaya za
Ushetu na Shinyanga.
Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa
wote, alipokuwa akiwaapisha kuwa wafanya uchunguzi kuhusu uwapo wa
watumishi hewa katika mikoa yao na kutoa taarifa.
Kutokana na
kutoa taarifa hizo zisizo za kweli, Jumatatu wiki hii, Rais Magufuli
alitangaza kutengua uteuzi wake, akiwa amekaa kwenye nafasi hiyo kwa
siku 27. Kilango amekuwa mkuu wa mkoa wa 19 tangu kuanzishwa kwa mkoa
huo.
Mbali na Kilango, Rais Magufuli pia alimsimamisha kazi
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Abdul Dachi, kutokana na taarifa
hizo za kutokuwapo watumishi hewa katika mkoa.
ALIYOSEMA KANISANI Akiwasalimia
waumini wenzake juzi, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, mjini Shinyanga,
baada ya kupewa fursa ya kusema neno, Kilango alisema anamshukuru Mungu
kwa kila jambo kwa yote yaliyomtokea.
“Ndugu waumini wenzangu,
hili ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu. Hata mtu unapojifungua mtoto
akafariki dunia, unamshukuru Mungu kwani hayo ni mapenzi ya Mungu.
"Ukiona
mzazi wako kafariki dunia pia, unamshuruku Mungu. Tunao wajibu wa
kumshukuru Mungu kwa kila jambo,” alisema kwa maneno mafupi na kisha
kuketi, huku akiacha simanzi miongoni mwa waumini wenzake, wakiwamo
viongozi wa kanisa.
ALIVYOANZA KAZI Mbele ya kikao
cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), muda mfupi baada ya kuanza kazi,
Kilango alisema Shinyanga ni mkoa wenye changamto nyingi ambazo
atazishughulikia, lakini atakuwa akilazimika kukimbia Dar es Salaam
kumwona mwenzi wake, Mzee John Malecela ambaye ni mgonjwa, na pindi hali
yake ikiimarika wataungana naye mjini Shinyanga.
Hayo aliyasema Machi 22, mbele ya wajumbe wa kikao cha kamati hiyo na Ijumaa Machi 25, alisali kanisani hapo.
Sambamba
na hayo, aliahidi kupambana na watumishi wazembe na wale wanaoendekeza
rushwa na ufisadi na kurejesha hadi ya mkoa wa Shinyanga kimaendeleo.
Kilango
ambaye yuko mjini Shinyanga, akisubiri kukabidhi ofisi kwa mrithi wake
kwa mujibu wa utaratibu, bado anaishi hotelini kwa vile aliyekuwa Mkuu
wa Mkoa huo, Ally Rufunga, hajaondoka katika nyumba ya serikali iliyoko
Ikulu ndogo, eneo la Lubaga.
ALICHOKISEMA MAGUFULI Wakati
akipokea hundi ya Sh. bilioni sita kutoa kwa Naibu Spika wa Bunge, Dk.
Tilia Ackson, Rais Magufuli alisema aliwapa wakuu wa mikoa siku 15
wakasimamie watumishi hewa, ambazo zilimalizika Machi 31, mwaka huu.
Alisema katika siku hizo 15, aliwaruhusu kufanya kazi hiyo kwa uhuru na
kuwaahidi hakutatokea kitu chochote na kwamba walifanya kazi vizuri.
Rais
Magufuli alisema watumishi hewa waliopatikana ni 5,507 ambao walikuwa
wanalipwa mishahara na miongoni mwao walikuwamo wanafunzi, waliokufa na
waliofungwa.
Alisema serikali imekuwa ikitenga Sh. bilioni 583 kulipa mishahara na kati ya fedha hizo hulipwa watumishi hewa.
“Ninaamini uchambuzi utaendelea kufanyika ili kuokoa mabilioni ya
fedha. Wizara ya Utumishi na ya Fedha muendelee kufanya kazi hiyo,”
alisema Magufuli.
Alisema zaidi ya Sh. bilioni 53 zilikuwa zinapotea kwa kuwalipa watumishi hewa 5,507.
Rais
Magufuli alisema watumishi hewa hawako katika halmashauri tu, bali wako
kila idara ya serikali, zikiwamo Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu,
vyombo vya ulinzi na usalama, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto na hata Wizara ya Fedha na Mipango.
Alisema
wakati akiwaapisha wakuu wa mikoa kwa kutambua tatizo hilo kuwa ni
kubwa, aliwapa agizo hilo na wengi waliitikia wito na kufanya kwa
ufanisi.
Rais Magufuli alisema akiwa wilayani Chato, aliona
taarifa zikitolewa na wakuu wa mikoa kuhusu watumishi hewa, lakini
alishangaa kusikia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga (Kilango), akisema katika
mkoa wake hakuna mtumishi hewa hata mmoja.
“Nilijiuliza ni
kweli? Nikatoa maagizo nikiwa Chato kuwa watu waende 'ku-verify'
(kuthibitisha) katika kila wilaya kama kweli hakuna watumishi hewa. Hadi
jana usiku (Jumapili usiku) walipatikana watumishi hewa 45 na bado
wilaya mbili zilikuwa hazijahakikiwa,” alisema.
“Niilijiuliza
sana, nikajiuliza sana na kweli nilijuliza maswali mengi kwa masikitiko
mengi kwa nini mkuu wa mkoa alizungumza vile wakati hakukuwa na adhabu
yoyote, lengo lake lilikuwa nini?
“Je, kama ni mkuu wa wilaya au
wasisidizi wake walimdanganya kwa nini na yeye alidanganya, ni shetani
gani aliyemkumba? “Nimeamua nitengue uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga
na atapangiwa kazi nyingine pamoja na katibu tawala wa mkoa,” alisema
Maguful
Basi moja la uchukuzi limechomwa
moto mjini Bujumbura Burundi na waandamanaji waliorejea mabarabarani
kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Waandamanaji wanachoma moto magurudumu haswa katika eneo la Kanyosha.
Kitongoji hicho kimekuwa kitovu cha maandamano haya dhidi ya awamu ya tatu ya rais Nkurunziza. .
Mwandishi wa BBC mjini Bujumbura Ismael Misigaro amesema milio ya risasi inasikika mjini humo.
Maandamano
haya yanarejea baada ya kuuawa kwa kiongozi wa chama cha upinzani Zedi
Feruzi nje ya nyumba yake katika mji mkuu Bujumbura.
Aidha
wanaharakati wa upinzani nchini humo wamesitisha mazungumzo na serikali
rais Pierre Nkurunziza ya kutaka kutanzua mzozo ulioko wa kisiasa.
Wandamanaji wakienderea na uchomaji matairi ya gari.
.
Mzozo huo unafuatia hatua ya Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Uamuzi
ambao wengi wanasema kuwa unaenda kinyume na sheria na ndio
iliyosababisha kuwepo kwa jaribio la kumpindua, na maandamano ya wiki
kadhaa.
Tayari zaidi ya raia 100,000 wa taifa hilo wametorokea mataifa jirani.
Kiongozi wa Mashtaka ametoa ruhusa ya kushtakiwa kwa mwaziri wanne
Kutumia ujumbe kwa vyombo vya
habari, mkuu wa mashtaka ya umma nchini Kenya Keriako Tobiko, hii leo
amevumbua yaliyomo katika hati za kesi za mawaziri wanne.
Tume ya
maadili na kupambana na ufisadi ya Kenya imependekeza waziri wa uchukuzi
mMhandisi Michael Kamau na waziri wa leba Kazungu Kambi kushtakiwa na
matumizi mabaya ya ofisi.
Mhandisi Michael Kamau anakumbwa na
shutuma za kutumia fedha ubadhirifu wa fedha za umma na kufanya
mabadiliko katika ubunifu wa barabara ambayo tiyari ilikuwa
imetengenezwa na mashauri.
Kazungu Kambi naye anadaiwa keteuwa wanachama wawili katika bodi ya shirika la taifa la hazina ya uzeeni kinyume na sheria.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana alasiri jumapili, afisa mkuu wa tume ya
maadili na kupambana na ufisadi Halakhe Waqo, alisema kwamba mawaziri
wanne waliochunguzwa ni waziri wa Uchukuzi Mhandisi Michael Kamau,
waziri wa ardhi, makao na ustawi wa miji bi Charity Ngilu, waziri wa
kilimo Felix Kosgei, waziri wa leba Kazungu kambi, seneta wa Nairobi
Mike Sonko na mbunge .
Tume hio imemwandikia rais Uhuru Kenyatta ombi la kuongeza muda wa uchunguzi wa kesi zilizobaki.
Siku sitini ambazo walikuwa wamepewa kukamilisha uchunguzi wa ripoti hiyo zimetimia leo.
Rais Uhuru Kenyatta alikuwa ametoa makataa ya siku 60 kushtakiwa kwa maafisa wakuu serikalini wafisadi
''Tumekuwa na shinikizo la
kukamilisha kesi kwa wakati uliotolewa ila wajibu wetu wa kufanya
uchunguzi wa kina ambao unaweza kustahimili uchunguzi mahakamani
umetulazimu kuomba muda zaidi''alisema Halakhe Waqo
Kwa sasa
tume hio imekamilisha kesi 56 kati ya 124 zilizowasilishwa kwa
uchunguzi zaidi baada ya ripoti yao ya awali iliyokabidhiwa rais
Kenyatta kuwasilishwa bungeni .
Kesi 21 tayari zimefikishwa kwa mkuu wa mashtaka ya umma Keriako Tobiko.
Kufikia
sasa maafisa 19 wamefikishwa mahakamani na wengine 29, kulingana na
afisa mkuu wa EACC, watafikishwa mahakamani siku chache zijazo katika
maeneo kadhaa nchini yakiwemo Turkana, Machakos, Nyamira, Nairobi na
Trans nzoia
Hata hivyo tume hii nayo pia imekumbwa na malumbano ya
ndani kwa ndani ya shtuma za ufisadi, zilizosababisha kuchunguzwa kwa
kiongozi wa tume hiyo na baadhi ya wanatume wake ambao hatimae
walijiuzulu.