HATIMA YA JAMES LEMBELI KURUDI CCM HII HAPA ISOME.

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na Mbunge wa zamani wa Kahama James Lembeli ambaye ni mwanachama wa Chadema mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano mjini Kahama mkoani Shinyanga.



Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mbunge wa zamani wa Kahama James Lembeli mara baada ya kuwasalimia wananchi waliofika kwa ajili ya kumsikiliza Rais katika viwanja hivyo vya Kahama.

Wakati jana Rais Magufuli akiwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga alimpa nafasi aliyekuwa Mbunge wa Kahama kwa tiketi ya CCM na baadae kuhamia CHADEMA, James Lembeli ili azungumze. 



Lembeli aliongea mambo kadhaa ikiwemo hatma yake kurudi CCM ambapo alisema yupo tayari kurudi iwapo Rais Magufuli atakisafisha chama kwa kuwashughulikia wanafiki na wala rushwa


Hapa chini ni maneno ya James Lembeli katika mkutano huo.

MAWAZIRI WAWILI WANUSULIKA KUTUMBULIWA NA RAIS MAGUFURI



 Operesheni ya kutumbua majipu ya Rais John Magufuli nusura iwaangukie Mawaziri wawili ambao  pia walikuwa  manaibu  mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Taarifa kutoka katika chanzo cha kuaminiwa zimeeleza kuwa Rais Magufuli alionesha kutoridhishwa na utendaji wa Mawaziri hao na kuwafokea mbele ya mawaziri wenzao  kwa kuwataja majina katika kikao maalum cha mawaziri kilichofanyika hivi karibuni.
"Ni mazingira ambayo mawaziri hawakuyazoea kwamba Rais anawaambia moja kwa moja kwa majina, anafoka akisema anaweza kuwafukuza wakati wowote.....
"Mawaziri wamezoea mara kwa mara wanapofanya kosa au uzembe wanaonywa kwa staili tofauti, ni kama ya kistaarabu hivi. Sasa huyu bwana mkubwa hana mchezo, aliwataja kabisa, tena mbele ya wenzao ambao walibaki vinywa wazi.

“Wewe (anataja jina la Waziri) na mwenzako (anamtaja jina pia) nitawatumbua,” Chanzo cha gazeti la Rais Mwema kinamkariri Rais Magufuli.
Mawaziri hao ambao ni wabunge wa kuchaguliwa majimboni kwa upande wa Tanzania Bara, wanaongoza wizara nyeti ambazo zinasimamia sekta mtambuka, wizara ambazo zinagusa sehemu ya ahadi za mabadiliko alizonadi Magufuli wakati akigombea urais katika kampeni za mwaka jana.

Chanzo hicho kilieleza kuwa Rais Magufuli aliwaonya pia mawaziri wengine ambao alionesha kutoridhishwa na utendaji wao kwakuwa hawaendani na kasi yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

“Magufuli alitaka atoe mfano kwa mawaziri wengine kwamba wao si watu maalum sana. Kama wanavyotumbuliwa watu wengine na wao pia wanaweza kutumbuliwa,” kiliongeza chanzo hicho

Rais Magufuli aliunda Baraza lake la Mawaziri mwishoni mwa mwaka jana na kuwashauri wasifanye sherehe ya kuteuliwa kwakuwa wakifanya vibaya hatawaonea haya atawaondoa mara moja bila kujali majina yao.

Utendaji wa Rais Magufuli umeendelea kusifiwa kila kona hususan katika kuwawajibisha viongozi wa ngazi zote na kuonesha nia ya dhati ya kuwahudumia watanzania huku akipambana na uzembe na ufisad

FIGISU ZA WABONGO HAZINAGA MWISHO DIVAS WA BONGO FLAVA, VANESSA MDEE NA SHILOLE WAINGIA KWENYE BIFU ZITO

divas






Bado kisa na mkasa hakijabainika wazi lakini ni Shishi ndiye aliyeanza kumtupia maneno Vee Money kwenye Instagram. Kuna uwezekano mkubwa wawili hao walizinguana nyuma ya pazia kabla ya kuamua kuumwaga ubuyu mtandaoni.
“Vee Jipange sana mwenzio Igunga niliaga sijaletwa kwa kubebwa kwenye lori, nimekuja na mbio za mwenge,” aliandika Shilole kwenye post ya Instagram ambayo imefutwa tayari. “We si wa magorofani na kiingereza chako cha kuunga, mi ndio mtoto wa mbwa sasa maninaa,” aliongeza Shilole.
Vanessa hakukaa kimya, alimjibu Shishi kwa post ambayo aliifuta muda mfupi baadaye. Akipost picha ya Shishi, Vee aliandika: Nikupe Kickiii ujulikane au sio? Kila siku twanyamaza ndio mtugaraze. Sit the f*ck down. Mimi sio wale uliowazoea. Ps: You ain’t worth this post inashushwa sasa hivi #MessageSent.
Haijashia hapo. Shilole amepost video akimpa ujumbe mwingine mkali zaidi muimbaji huyo wa ‘Niroge.’
“Vanessa nimepata ujumbe wako wa Kiingereza japokuwa nimeusoma kwa tabu sana lakini nimepata baadhi baadhi,” anasikika akisema kwenye video hiyo.

“Listen to me my sister, you see me nah, mimi mwenzio nimezaliwa Igunga, nimezoea kula ugali, sijazoea kula chips mayai kama unavyokula wewe. So mama ninapiga kuliko maelezo, usiombe kukutana na mimi, au waulize wenzio waliokutana na vibao vyangu wanaweza kukuambia kwamba kibao cha Shishi ukikutana nacho lazima uombe Panadol,” anaonya Shishi.“Aisee bibi, bibie, bibie, I am telling you yaani usiombe kukutana na Bi Shishi, yaani usiombe ukakutana na mimi tit for tat, yaani mama Kiingereza chako nimekiona, jipange, I am telling you, If I see you me and you.”
Acha tuone movie hii itaishia wapi. Lakini kwa vitisho hivyo Vanessa hana budi kuwa na bodyguard wake sasa
ANNA KILANGO AIBUKIA KANISANI NA KUTOA YA MOYONI BAADA YA KUTIMULIWA UKUU WA MKOA SHINYANGA

ANNA KILANGO AIBUKIA KANISANI NA KUTOA YA MOYONI BAADA YA KUTIMULIWA UKUU WA MKOA SHINYANGA

ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela, (Pichani) ameibukia kanisani na kutoa ya moyoni, ikiwa siku tano baada ya Rais Dk. John Magufuli kutengua uteuzi wake.

Kilango, ambaye Jumatatu wiki hii uteuzi wake ulitenguliwa baada ya Machi 20, mwaka huu, kudai kuwa mkoa wa Shinyanga hauna mtumishi hewa wa serikali hata mmoja.

Hata hivyo, Ikulu ilifanya uchunguzi na kubaini kuwa katika taarifa za awali kuna watumishi hewa 45, huku kazi ya uhakiki ikiendelea katika wilaya za Ushetu na Shinyanga.

Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa wote, alipokuwa akiwaapisha kuwa wafanya uchunguzi kuhusu uwapo wa watumishi hewa katika mikoa yao na kutoa taarifa.

Kutokana na kutoa taarifa hizo zisizo za kweli, Jumatatu wiki hii, Rais Magufuli alitangaza kutengua uteuzi wake, akiwa amekaa kwenye nafasi hiyo kwa siku 27. Kilango amekuwa mkuu wa mkoa wa 19 tangu kuanzishwa kwa mkoa huo.

Mbali na Kilango, Rais Magufuli pia alimsimamisha kazi Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Abdul Dachi, kutokana na taarifa hizo za kutokuwapo watumishi hewa katika mkoa.

ALIYOSEMA KANISANI
Akiwasalimia waumini wenzake juzi, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, mjini Shinyanga, baada ya kupewa fursa ya kusema neno, Kilango alisema anamshukuru Mungu kwa kila jambo kwa yote yaliyomtokea.

“Ndugu waumini wenzangu, hili ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu. Hata mtu unapojifungua mtoto akafariki dunia, unamshukuru Mungu kwani hayo ni mapenzi ya Mungu.

"Ukiona mzazi wako kafariki dunia pia, unamshuruku Mungu. Tunao wajibu wa kumshukuru Mungu kwa kila jambo,” alisema kwa maneno mafupi na kisha kuketi, huku akiacha simanzi miongoni mwa waumini wenzake, wakiwamo viongozi wa kanisa.

ALIVYOANZA KAZI
Mbele ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), muda mfupi baada ya kuanza kazi, Kilango alisema Shinyanga ni mkoa wenye changamto nyingi ambazo atazishughulikia, lakini atakuwa akilazimika kukimbia Dar es Salaam kumwona mwenzi wake, Mzee John Malecela ambaye ni mgonjwa, na pindi hali yake ikiimarika wataungana naye mjini Shinyanga.

Hayo aliyasema Machi 22, mbele ya wajumbe wa kikao cha kamati hiyo na Ijumaa Machi 25, alisali kanisani hapo.

Sambamba na hayo, aliahidi kupambana na watumishi wazembe na wale wanaoendekeza rushwa na ufisadi na kurejesha hadi ya mkoa wa Shinyanga kimaendeleo.

Kilango ambaye yuko mjini Shinyanga, akisubiri kukabidhi ofisi kwa mrithi wake kwa mujibu wa utaratibu, bado anaishi hotelini kwa vile aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Ally Rufunga, hajaondoka katika nyumba ya serikali iliyoko Ikulu ndogo, eneo la Lubaga.

ALICHOKISEMA MAGUFULI
Wakati akipokea hundi ya Sh. bilioni sita kutoa kwa Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tilia Ackson, Rais Magufuli alisema aliwapa wakuu wa mikoa siku 15 wakasimamie watumishi hewa, ambazo zilimalizika Machi 31, mwaka huu.
Alisema katika siku hizo 15, aliwaruhusu kufanya kazi hiyo kwa uhuru na kuwaahidi hakutatokea kitu chochote na kwamba walifanya kazi vizuri.

Rais Magufuli alisema watumishi hewa waliopatikana ni 5,507 ambao walikuwa wanalipwa mishahara na miongoni mwao walikuwamo wanafunzi, waliokufa na waliofungwa.

Alisema serikali imekuwa ikitenga Sh. bilioni 583 kulipa mishahara na kati ya fedha hizo hulipwa watumishi hewa.
“Ninaamini uchambuzi utaendelea kufanyika ili kuokoa mabilioni ya fedha. Wizara ya Utumishi na ya Fedha muendelee kufanya kazi hiyo,” alisema Magufuli.

Alisema zaidi ya Sh. bilioni 53 zilikuwa zinapotea kwa kuwalipa watumishi hewa 5,507.

Rais Magufuli alisema watumishi hewa hawako katika halmashauri tu, bali wako kila idara ya serikali, zikiwamo Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, vyombo vya ulinzi na usalama, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na hata Wizara ya Fedha na Mipango.

Alisema wakati akiwaapisha wakuu wa mikoa kwa kutambua tatizo hilo kuwa ni kubwa, aliwapa agizo hilo na wengi waliitikia wito na kufanya kwa ufanisi.

Rais Magufuli alisema akiwa wilayani Chato, aliona taarifa zikitolewa na wakuu wa mikoa kuhusu watumishi hewa, lakini alishangaa kusikia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga (Kilango), akisema katika mkoa wake hakuna mtumishi hewa hata mmoja.

“Nilijiuliza ni kweli? Nikatoa maagizo nikiwa Chato kuwa watu waende 'ku-verify' (kuthibitisha) katika kila wilaya kama kweli hakuna watumishi hewa. Hadi jana usiku (Jumapili usiku) walipatikana watumishi hewa 45 na bado wilaya mbili zilikuwa hazijahakikiwa,” alisema.

“Niilijiuliza sana, nikajiuliza sana na kweli nilijuliza maswali mengi kwa masikitiko mengi kwa nini mkuu wa mkoa alizungumza vile wakati hakukuwa na adhabu yoyote, lengo lake lilikuwa nini?

“Je, kama ni mkuu wa wilaya au wasisidizi wake walimdanganya kwa nini na yeye alidanganya, ni shetani gani aliyemkumba? “Nimeamua nitengue uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga na atapangiwa kazi nyingine pamoja na katibu tawala wa mkoa,” alisema Maguful
WATU 430 NCHINI INDIA WAAGA DUNIA KWA KUKUMBWA NA WIMBI LA JOTO KUBWA

WATU 430 NCHINI INDIA WAAGA DUNIA KWA KUKUMBWA NA WIMBI LA JOTO KUBWA

.
Takriban watu 430 wamekufa kutokana na wimbi la joto linalovuma nchini India.
Watafiti wamesajili kiwango cha juu mno cha nyuzijoto 48'C katika maeneo mengi nchini humo.
Vifo vingi zaidi vimeripotiwa katika majimbo ya kusini ya Telangana na Andhra Pradesh, ambapo watu 140 wamepoteza maisha yao kuanzia jumamosi wimbi hilo la joto lilipotokea.
Mji wa Allahabad ulioko Uttar Pradesh ulisajili vipimo vya nyuzijoto 48C huku wakaazi wa mji mkuu wa India New Delhi ukistahimili kiwango cha nyuzijoto 44C .
.
Maafisa wa utawala nchini humo wameanza kampeini ya kuwahamasisha wanainchi kukaa majumbani mwao na kuwashauri wanye waji mengi.
Yamkini viwango vya joto vimekuwa juu zaidi katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita lakini vifo vimeanza kuripotiwa mwishoni mwa juma.
Jimbo la Andhra Pradesh ndilo lililopoteza watu wengi zaidi ikiwa na jumla ya watu 246 waliopoteza maisha yao kuanzia juma lililopita.
Jimbo la Andhra Pradesh ndilo lililopoteza watu 
.
asilimia kubwa ya wale waliopoteza maisha ni watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 walioshinda nje ya majumba yao.'' alisema kamishna wa kupambana na majanga katika jimbo la Andhra Pradesh.
Wakfu wa waandishi wa habari wanasema kuwa watu 186 wameaga katika wilaya 10 za jimbo la Telangana.
Watu 58 wamekufa kuanzia siku ya jumamosi.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa imesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa hali hiyo ya joto kuendelea kwa siku kadha zijazo.
Wenyeji waamua kuakaa ndani na kuamua kunywa maji tu.
 .
Watu wengine kumi walpoteza maisha yao katika jimbo la Magharibi mwa Bengal.
Waendesha teksi ambazo hazina kiyoyozi hawataruhusiwa kuhudumu kwa saa tano katika mji mkuu wa Kolkata. Hii inafuatia vifo vya madereva wawili.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa inasema kuwa hali hiyo ya juu ya joto inatokana na ukosefu wa mvua.


WANAJESHI 7 WAUWAWA UKO TUNISIA.

WANAJESHI 7 WAUWAWA UKO TUNISIA.

.
Mwanajeshi mmoja nchini Tunisia amempigwa risasi na kuuawa baada ya kuwaua wenzake 7 .
Askari wengine 10 walijeruhiwa mmoja wao akiwa hali mahututi katika shambulizi lililotokea katika hafla ya kupeperusha bendera katika kambi ya kijeshi ya Bouchoucha.
Kwa mujibu wa msemaji wa idara ya ulinzi Belhassen Oueslati askari huyo alikuwa na matatizo ya kifamilia na kiakili.
Wakati wa tukio afisa huyo alikuwa amekatazwa kubeba silaha yeyote.
Duru zinasema kuwa askari huyo alimiminiwa risasi na kuuawa pia na wenzake, ili kumzima asiendelee kutekeleza maafa hayo kisha utulivu ukarejelewa.
Wakuu wamekanusha kuwa kisa hicho kilichofanyika katika kambi moja ya kijeshi mjini Tunis, sio ya kigaidi.
Lakini kilisababisha taharuki kubwa mjini humo, ambapo mnamo mwezi Machi, wapiganaji wa kiislamu waliokuwa na silaha waliwauwa zaidi ya watu 20, wengi wao watalii, baada ya kuvamia makavadhi ya Bardo mjini Tunis.
Bwana Ouselati alisema kuwa afisa huyo alimshambulia afisa mmoja kwa kisu kabla ya kumpokonya bunduki na kuitumia kuwashambulia maafisa wengine.
Aliongezea kusema kuwa ''ninahakika kuwa hilo lilikuwa tukio la kipekee wala sio la kigaidi''
MAGARI YAZIDI CHOMWA MOTO BURUNDI HALI BADO NI TETE.

MAGARI YAZIDI CHOMWA MOTO BURUNDI HALI BADO NI TETE.

.
Basi moja la uchukuzi limechomwa moto mjini Bujumbura Burundi na waandamanaji waliorejea mabarabarani kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Waandamanaji wanachoma moto magurudumu haswa katika eneo la Kanyosha.
Kitongoji hicho kimekuwa kitovu cha maandamano haya dhidi ya awamu ya tatu ya rais Nkurunziza.
.
Mwandishi wa BBC mjini Bujumbura Ismael Misigaro amesema milio ya risasi inasikika mjini humo.
Maandamano haya yanarejea baada ya kuuawa kwa kiongozi wa chama cha upinzani Zedi Feruzi nje ya nyumba yake katika mji mkuu Bujumbura.
Aidha wanaharakati wa upinzani nchini humo wamesitisha mazungumzo na serikali rais Pierre Nkurunziza ya kutaka kutanzua mzozo ulioko wa kisiasa.
Wandamanaji wakienderea na uchomaji matairi ya gari.
.
Mzozo huo unafuatia hatua ya Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Uamuzi ambao wengi wanasema kuwa unaenda kinyume na sheria na ndio iliyosababisha kuwepo kwa jaribio la kumpindua, na maandamano ya wiki kadhaa.
Tayari zaidi ya raia 100,000 wa taifa hilo wametorokea mataifa jirani.


NITAONDOKA TUWESTHAM:SAM ALLARDYCE AFUNGUKA

NITAONDOKA TUWESTHAM:SAM ALLARDYCE AFUNGUKA

.
Kocha wa timu ya soka ya West Ham United ya England Sam Allardyce amefichua mpango wake wa kuondoka klabuni hapo hata kama timu hiyo ilimpa nafasi ya mkataba mpya.
Taarifa za kuondoka kwa Allardyce zilitangazwa dakika za mwisho za mechi kati ya West Ham dhidi ya Newcastle United, mtanange ambao uliisha kwa ushindi wa bao mbili kwa bila walioupata Newcastle na kujinasua katika janga la kushuka daraja. Allardyce ametumia miaka minne kuifundisha West Ham lakini wagonga nyundo hao wameamua kutompa tena mkataba mpya katika majira haya ya joto. "sikutaka kubaki, naweza sema kama tulikuwa tunafikra sawa kama na wao hawakuwa wenye kunihitaji pia" alisema Kocha huyo.
REALMADRID YAMTIMUWA CARLO ANCELOTTI

REALMADRID YAMTIMUWA CARLO ANCELOTTI

.
Hatimaye miamba ya soka nchini Hispania Real Madrid imemtimua kocha wa timu hiyo Carlo Ancelotti baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa misimu miwili.
Kocha huyo raia wa Italia, aliiongoza Madrid kutwaa taji la kombe la Hispania kabla ya kuibebesha miamba hiyo taji la kumi la klabu bingwa barani Ulaya. Pamoja na mafanikio hayo aliyoyapata msimu uliopita, mwaka huu haukuwa mzuri kwa vijana hao wa Benabeu baada ya kuambulia patupu kwa kukosa hata kombe moja japokuwa kikosi cha timu hiyo kinatajwa kuwa cha gharama ya juu. Hasira za viongozi wa klabu hiyo ziliongezeka baada ya kutupwa nje na Juventus katika hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya huku wapinzani wao wakubwa Barcelona ikinyakuwa taji la ligi kuu na kutinga fainali ya klabu bingwa na kombe la Hispania. Rais wa Madrid Florentino Perez amewaambia waandishi wa habari kuwa haikuwa rahis kumtema kocha huyo na kuongeza kuwa kocha mpya atateuliwa wiki ijayo.
PAPAFRANCIS: SIJATAZAMA TV KWA MIAKA 25.

PAPAFRANCIS: SIJATAZAMA TV KWA MIAKA 25.

.
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, amesema kuwa hajawahi kutazama runinga kwa miaka 25 sasa.
Papa Prancis ambaye amewatamausha wachanganuzi wa kanisa hilo kwa kususia maisha ya kifahari katika makao makuu ya kanisa Vatican alisema alitizama runinga mara ya mwisho tarehe 15 mwezi julai mwaka wa 1990.
Alikoma kutizama runinga baada ya kumuahidi maria mtakatifu kuwa angekoma kushiriki uraibu huo.

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, amesema kuwa hajawahi kutizama runinga kwa miaka 25 sasa                                                                                                                                                                            
Isitoshe raia huyo wa Argentina amesema kuwa hatumii mtandao wa intaneti.
Na akitaka kupata habari za kimataifa , Papa anasema kuwa huwa anatenga dakika 10 tu ya muda wake kusoma gazeti la kiitaliano.
Papa Francis vilevile anafuatilia habari za klabu yake maarufu huko Argentina kupitia kwa wahudumu       

Papa Francis vilevile anafuatilia habari za klabu yake maarufu huko Argentina kupitia kwa wahudumu wake ambao humsimulia yanayojiri.
Je unaweza kukaa mbali na Runinga yako Simu yako ama mtandao wa Intanet japo kwa siku moja ?


UFISADI WAWAWEKA HATIANI WABUNGE WANNE KENYA.

UFISADI WAWAWEKA HATIANI WABUNGE WANNE KENYA.



Kiongozi wa Mashtaka ametoa ruhusa ya kushtakiwa kwa mwaziri wanne  
Kutumia ujumbe kwa vyombo vya habari, mkuu wa mashtaka ya umma nchini Kenya Keriako Tobiko, hii leo amevumbua yaliyomo katika hati za kesi za mawaziri wanne.
Tume ya maadili na kupambana na ufisadi ya Kenya imependekeza waziri wa uchukuzi mMhandisi Michael Kamau na waziri wa leba Kazungu Kambi kushtakiwa na matumizi mabaya ya ofisi.
Mhandisi Michael Kamau anakumbwa na shutuma za kutumia fedha ubadhirifu wa fedha za umma na kufanya mabadiliko katika ubunifu wa barabara ambayo tiyari ilikuwa imetengenezwa na mashauri.
Kazungu Kambi naye anadaiwa keteuwa wanachama wawili katika bodi ya shirika la taifa la hazina ya uzeeni kinyume na sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari jana alasiri jumapili, afisa mkuu wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi Halakhe Waqo, alisema kwamba mawaziri wanne waliochunguzwa ni waziri wa Uchukuzi Mhandisi Michael Kamau, waziri wa ardhi, makao na ustawi wa miji bi Charity Ngilu, waziri wa kilimo Felix Kosgei, waziri wa leba Kazungu kambi, seneta wa Nairobi Mike Sonko na mbunge .
Tume hio imemwandikia rais Uhuru Kenyatta ombi la kuongeza muda wa uchunguzi wa kesi zilizobaki.
Siku sitini ambazo walikuwa wamepewa kukamilisha uchunguzi wa ripoti hiyo zimetimia leo.

Rais Uhuru Kenyatta alikuwa ametoa makataa ya siku 60 kushtakiwa kwa maafisa wakuu serikalini wafisadi
''Tumekuwa na shinikizo la kukamilisha kesi kwa wakati uliotolewa ila wajibu wetu wa kufanya uchunguzi wa kina ambao unaweza kustahimili uchunguzi mahakamani umetulazimu kuomba muda zaidi''alisema Halakhe Waqo
Kwa sasa tume hio imekamilisha kesi 56 kati ya 124 zilizowasilishwa kwa uchunguzi zaidi baada ya ripoti yao ya awali iliyokabidhiwa rais Kenyatta kuwasilishwa bungeni .
Kesi 21 tayari zimefikishwa kwa mkuu wa mashtaka ya umma Keriako Tobiko.
Kufikia sasa maafisa 19 wamefikishwa mahakamani na wengine 29, kulingana na afisa mkuu wa EACC, watafikishwa mahakamani siku chache zijazo katika maeneo kadhaa nchini yakiwemo Turkana, Machakos, Nyamira, Nairobi na Trans nzoia
Hata hivyo tume hii nayo pia imekumbwa na malumbano ya ndani kwa ndani ya shtuma za ufisadi, zilizosababisha kuchunguzwa kwa kiongozi wa tume hiyo na baadhi ya wanatume wake ambao hatimae walijiuzulu.

WAKATI WANANCHI WANAZIDI TESEKA MHE: NKURUNZINZA AMUA KUINGIA KIWANJANI KUSAKATA KABUMBU.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza ameendelea na burudani ya kucheza mpira mjini Bujumbura nchini humo.Huku maandamano ya raia kupinga kugombea kwake awamu ya tatu yakiendelea nchini .Polisi wamekua wakizuia maandamano hayo na kuuwawa baadhi ya raia.Hata hivyo rais huyo ameonekana kutojali akiendelea na mambo yake.
DROGBA AIAGA CHELSEA UKU MASHABIKI WAKIMSHANGILIA

DROGBA AIAGA CHELSEA UKU MASHABIKI WAKIMSHANGILIA

WASOMI WASEMA: JK AONA MBALI JUU YA MAMBO MENGI HAPA NCHINI

WASOMI WASEMA: JK AONA MBALI JUU YA MAMBO MENGI HAPA NCHINI


Akizungumza jana, Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu), Gaudence Mpangala alisema mwaka huu CCM itakuwa na ushindani mkali kuliko ilivyowahi kutokea kwenye uchaguzi wowote wa nyuma.
Wasomi na wachambuzi wa siasa wamesema Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ameona mbali kuwataka viongozi wa chama hicho kuteua mgombea wa urais anayekubalika ndani na nje ya chama wakisema bila kufanya hivyo wataangushwa na mgombea wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Akizungumza jana, Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu), Gaudence Mpangala alisema mwaka huu CCM itakuwa na ushindani mkali kuliko ilivyowahi kutokea kwenye uchaguzi wowote wa nyuma.
Alisema ushindani huo unatokana na kuwapo kwa mgombea urais wa Ukawa unaoundwa na vyama Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD.
“Vyama hivyo vimeamua kushirikiana kusimamisha mgombea mmoja kwenye nafasi ya urais, ubunge na udiwani, ushirikiano huo utatoa upinzani mkali kwa CCM,” alisema Mpangala.
Alisema CCM wameliona hilo na ndiyo maana Rais Kikwete ameona ni muhimu awaeleze wana CCM kwamba wanatakiwa kuchagua viongozi wanaokubalika na wananchi walio wengi, vinginevyo watashindwa.
“Yale mambo ya zamani ya kila kundi kuwa na mgombea wake yakirudiwa hivi sasa yatakigharimu chama hicho, wanatakiwa kuungana na kuweka mtu anayekubalika bila kujali makundi,” alisema.
Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Alexander Makulilo pia alisema Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utakuwa na tofauti kubwa na chaguzi zilizopita, hivyo lazima wapate mgombea maarufu.
Akitoa mfano wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 alisema: “Katika kipindi hicho Mkapa (Benjamin) hakuwa akifahamika sana ukilinganisha na wana-CCM wengine waliokuwa wakiwania nafasi hiyo lakini alishinda na kuwa rais. Mwaka huu wakijaribu kufanya hivyo wataanguka vibaya, hali ya kisiasa imebadilika,” alisema.
Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, viashiria vinaonyesha kuwa vyama vya upinzani vinazidi kuwa na nguvu mwaka hadi mwaka, akitaja Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita kama mfano... “Hata mgombea wa urais wa CCM, 2010 alipata kura chache ikilinganishwa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Hii ina maana vyama vya upinzani vinakua kwa kasi,” alisema.
Alisema kukithiri kwa rushwa na umaskini katika jamii kumewakatisha tamaa wananchi hivyo watahitaji kiongozi mwenye uwezo kupunguza matatizo hayo.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Dk Emmanuel Malya alisema Rais Kikwete anafahamu kuwa chama hicho kisipoweka wagombea wanaokubalika kitaanguka kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
“Kikwete ameliona hilo na wanachama wenzake wafahamu kuwa huu si wakati wa kuweka mtu wao, bali mtu anayekubalika na wananchi walio wengi,” alisema.

RATIBA YA URAISI CC YATOKA.WAGOMBEA KUSAKA WADHAMINIi 450, FOMU KUANZA KUTOREWA Juni 3


MGOMBEA Urais kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) atajulikana Julai 12 mwaka huu baada ya kukamilisha mchakato mzima wa kuomba kuwania nafasi hiyo, kutafuta wadhamini na kujadiliwa katika chama hicho.
 
Hayo yalielezwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari kueleza yanayoendelea katika siku ya pili ya kikao hicho mjini hapa.
 
Alisema mchakato wa kupata wagombea wa CCM katika vyombo vya dola yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, wabunge, wawakilishi na madiwani kwa uchukuaji wa fomu utafanyika kuanzia Juni 3 hadi Julai 15 mwaka huu.
 
Gharama za fomu hizo hazijapanda zimebaki vile vile kama zilivyokuwa mwaka 2010 na katika kanuni, yaani shilingi milioni 1 kwa urais, shilingi laki moja kwa ubunge na elfu hamsini kwa diwani.
 
Akifafanua zaidi alisema kwamba, wagombea Urais wataanza kuchukua fomu,bila mbwembwe kuanzia Juni 3 na kutakiwa kurejesha fomu hiyo mwisho saa 10 ya Julai 2 mwaka huu katika mazingira hayo hayo ya kutokuwepo na shamrashamra.
 
Aidha alisema kuanzia tarehe hiyo ya uchukuaji fomu hadi marejesho yake, wagombea watakuwa wanatafuta wadhamini 450 kutoka mikoa 15 nchini huku mikoa mitatu ikiwa ni kutoka Zanzibar na angalau mkoa mmoja uwe wa Unguja au kisiwa cha Pemba.
 
Ongezeko hilo la mikoa na wadhamini linatokana na haja ya kutafuta sampuli inayooana na idadi ya watu na mikoa kwa sasa. Tanzania ina mikoa 31.
 
Uchaguzi uliopita wagombea walitakiwa kutafuta wadhamini 250 katika mikoa 10, minane ikiwa ni kutoka Bara. Alisema wagombea urais hao wanapokwenda kutafuta wadhamini, wajumbe wote wa mkutano mkuu wa taifa hawataruhusiwa kuwa wadhamini, huku mwanachama atakayekuwa mdhamini akizuiwa kufanya udhamini wa zaidi ya mtu mmoja.
 
Kwa anayewania Urais wa Zanzibar tarehe za kuchukua na kurejesha ni zile zile za Jamhuri, huku akitakiwa kupata wadhamini 250 kutoka mikoa mitatu, mmoja ukiwa ama Unguja au Pemba.
 
Alisema vikao vya kuchuja wagombea Urais Zanzibar vitafanyika kuanzia Julai 4 hadi 10 ambapo Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM itamtaja Mgombea Urais wa Zanzibar.
 
Aidha wajumbe wote wa NEC hawaruhusiwi kumdhamini mgombea Urais wa Zanzibar. Akizungumzia fomu za wagombea Ubunge, alisema kwamba wanachama watachukua fomu hizo Julai 15 na kuzirejesha Julai 19 na mikutano ya kampeni itafanyika kuanzia Julai 20-31 ili kuomba kura.
 
Kura ya maoni ya kuwapata wanaowania nafasi ya Ubunge kupitia CCM itafanyika Agosti 1, mwaka huu. 
 
Kwa wanaowania Viti Maalumu ratiba ni ile ile, lakini safari hii mchujo wa mwisho utafanywa na Baraza kuu la UWT ambao kimsingi ndio wanaomiliki viti hivyo maalumu, ingawa mchujo wa awali utafanyika katika jumuiya husika.
 
Viti maalumu safari hii vitawaniwa pia na jumuiya ya wazazi ambao wamepewa viti viwili.Jumuiya nyingine ni jumuiya ya vijana, UWT yenyewe,jumuiya ya wasomi, wafanyakazi na wenye ulemavu.
 
Ratiba ya kuwania udiwani nayo ni Julai 15 hadi 19 na kura za maoni zitafanyika Agosti Mosi. Katibu huyo wa NEC hata hivyo aliwatahadharisha wanaowania nafasi hizo za dola kupitia CCM, kuangalia kwa makini kanuni za uchaguzi za chamhamshatz.blogsport.coma hicho, kuzisoma na kuzielewa kwa kuwa kama watafanya kosa litawagharimu ,huku akisisitiza ‘kosa moja goli moja’.
 
Akizungumzia namna ya kufanikisha kura ya maoni alisema chama chake kitafunga daftari la wanachama Julai 15 na wapiga kura wa chama hicho watalazimika kuwa na zaidi ya kadi ya chama kwa utambulisho ikiwamo kadi ya kupiga kura ili kushiriki kura ya maoni.
 
Alisema nia ya kuweka vitambulisho viwili ni kuzuia wapiga kura bandia ambao safari iliyopita walionekana kuwa chanzo cha matatizo. Aidha, wanafanya hivyo ili kuzuia wasioitakia mema CCM kula njama ya kuiangusha kupitia matumizi ya kadi bandia.
 
Aidha alisema ipo mikakati ambayo tayari inafanyiwa kazi kuhakikisha mchakato mzima hadi kura wa maoni unafanikiwa kuwapa Watanzania kile wanachokihitaji.
 
Pia alisema wagombea wote watakuwa pamoja katika mikutano ya kuomba kura. 
 
Akijibu swali maana ya maelekezo ya sasa kama ni hakikisho Katiba mpya haitakuwepo, Nape alisema CCM inafanya utaratibu wake kwa kuzingatia Katiba iliyopo sasa na kama katiba mpya itakuja watakutana kufanya mabadiliko yanayohitajika.

JIONEE MATUKIO MBALIMBALI YA MKUTANO WA CHADEMA ULIOFANYIKA JANA TANGANYIKA PACKERS KAWE Jijini Dar


Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Mh.Freeman Mbowe akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Parkers Jana, ambapo pia alizindua kitabu cha Mbunge wa jimbo la Kawe Mh. Halima Mdee.
 Mh Freeman Mbowe, Halima Mdee na John Mnyika wakizindua kitabu cha Mbunge wa Kawe Mh Halima Mdee
 Gwajima akiwa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA
 Mchungaji Gwajima akiongozwa na Halima Mdee kwenye jukwaa kuu
 Wafuasi wa CHADEMA wakisikiliza hotuba ya mwenyekiti wao, Freeman Mbowe
Umati wa watu waliohudhuria mkutano wa CHADEMA uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers.

CHADEMA YARAHANI VIKALI SHERIA INAYO NYIMA UHURU VYOMBO VYA HABARI HAPA NCHINI.

Dk. Wilibroad Slaa akizungumzia juu sheria iyo mjini bukoba.hamshatz.blogsport.com

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka watanzania kuipinga na kutoikubali sheria  ya mpya iliyopitishwa ya takwimu kwa madai kwamba sheria hiyo inalenga kuzuia uhuru wa vyombo vya habari na kuwanyima watanzania haki na uhuru wa kupata habari.
 
Akihutubia hivi karibuni mjini Bukoba  katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dk. Wilibroad Slaa alisema kupitishwa kwa sheria hiyo kunalenga kunyima uhuru wa habari pamoja na kuwafanya watanzania kuendelea kubaki gizani na kuishi kama wapo  shimoni bila kuelewa maovu yanayofanywa na viongozi wasio waadilifu wanaotumia madaraka vibaya kwa masalahi yao binafsi.
 
Alisisitiza kuwa  nia ya serikali kutaka kuzuia uhuru wa vyombo vya habari ni kuwarudisha nyuma watanzania ili waweze kuishi bila kupata habari kama ilivyokuwa enzi za ukoloni na kwamba hali hiyo haiwezi kuvumiliwa kwani serikali inataka kuficha maovu ambayo yanaweza   kuliangamiza taifa hapo baadae.

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM -BARA,MWIGULU NCHEMBI AMEJIUZURU WADHIFA HUO KUTOKANA KUA ANATAKA KUGOMBEA WADHIFA MWINGINE.


Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba
----
Aliyekua Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara,Mwigulu Nchemba amejiuzulu wadhifa huo.
 
Mwigulu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha,ametangaza kujiuzulu nafasu hiyo  jana Jioni katika kikao cha Halmashauri Kuu ya ya Taifa ya CCM,Mjini Dodoma

Akithibiths tukio hilo,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi ,Naoe Nnauye amesema,Mwigulu ameamua kujiuzulu nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara kutokana na nia yake ya kutaka kuomba kuwania Urais kwa tiketi ya CCM  katika Uchaguzi utakaofanyika Octoba Mwaka huu

"Mwigulu alishamwambia nia hiyo Mwenyekiti wa Chama  Rais Jakaya Kikwete,nae Rais akamkubalia, na sasa  katika kikao ameomba rasmi kujiuzulu na Mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete amemkubalia Mbele ya wajumbe wa NEC".amesema Nape

Nape amesema kufuatia uamuzi wa mwigulu  kujiuzulu, Mwenyekiti wa Chama Rais Jakaya Kikwete amemteua Msaidizi wake wa maswala ya siasa,Rajabu Ruhavi kuwa Mjumbe wa NEC na Wakati huohuo kamteua kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara Kushika nafasi iliyoachwa na Mwigulu Nchemb 

JWTZ YATOA SUPRISE KWA WANASONGEA BAADA YA KUPITISHA HAMSHA HAMSHA BILA WAO KUJUA

Chini ya  Brigedia Jenerali wa Kamandi ya Kusini, John Chacha

Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wilayani Songea jana limezua kizaa zaa kwa wananchi kufuatia kuvamia mitaani, maofisini (serikali na binafsi) makanisani na misikitini wakiwa na silaha huku magari yao yakiranda kila kona na kuanza upekuzi  kwa watu wote walokutana nao huku wakidai kuonyeshwa vitambulisho.
 
Aidha,indaiwa kuwa baadhi ya wakazi wa mjini hapo waliamua kujifungia ndani huku wengine wakisema kwamba jeshi hilo linawasaka  magaidi waliovamia katika mji wa Songea kutokana na jeshi hilo kutowafahamisha wananchi nini hasa dhumuni la msako huo.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela alipoulizwa alisema zoezi hilo ni la kawaida  huku akiwataka wakazi wa mjini songea  kuwa na amani na waendelee kufanya shughuli zao kama kawaida.
 
Naye  Brigedia Jenerali wa Kamandi ya Kusini, John Chacha alisema hiyo ni sehemu ya mafunzo kwa wanajeshi hao na kuongeza kuwa  jeshi hilo  hufanya mafunzo mbalimbali ya kujiimarisha ikiwamo ya kulinda miji, maporini na mengineyo.

Kategori

Kategori