Kocha wa timu ya soka ya West Ham
United ya England Sam Allardyce amefichua mpango wake wa kuondoka
klabuni hapo hata kama timu hiyo ilimpa nafasi ya mkataba mpya.
Taarifa
za kuondoka kwa Allardyce zilitangazwa dakika za mwisho za mechi kati
ya West Ham dhidi ya Newcastle United, mtanange ambao uliisha kwa
ushindi wa bao mbili kwa bila walioupata Newcastle na kujinasua katika
janga la kushuka daraja. Allardyce ametumia miaka minne kuifundisha West
Ham lakini wagonga nyundo hao wameamua kutompa tena mkataba mpya katika
majira haya ya joto. "sikutaka kubaki, naweza sema kama tulikuwa
tunafikra sawa kama na wao hawakuwa wenye kunihitaji pia" alisema Kocha
huyo.
Mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba anaihama klabu hiyo kwa mara ya pili.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alisajiliwa na klabu hiyo mwaka 2004 na amefunga mabao 164 katika mechi 381.Ningependa kucheza tena kwa msimu mmoja zaidi na kwa hilo kufanikiwa itabidi nihamie kilabu nyengine aliuambia mtandao wa Chelsea.
Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho alimsajili kwa mara ya pili Drogba kwa kandarasi ya mwaka mmoja baada ya kuondoka Galatasaray.



Na hapo yuko anaonyesha manjonjo na kupiga contro je?wananchi wana aja na kutazama umaili wa kucheza mpira.



m
.jpg)
