Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na
Mbunge wa zamani wa Kahama James Lembeli ambaye ni mwanachama wa
Chadema mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano mjini Kahama mkoani
Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John
Pombe Magufuli akimpongeza Mbunge wa zamani wa Kahama James Lembeli mara
baada ya kuwasalimia wananchi waliofika kwa ajili ya kumsikiliza Rais
katika viwanja hivyo vya Kahama. Wakati jana Rais Magufuli akiwa
wilayani Kahama mkoani Shinyanga alimpa nafasi aliyekuwa Mbunge wa
Kahama kwa tiketi ya CCM na baadae kuhamia CHADEMA, James Lembeli ili
azungumze.
Lembeli aliongea mambo kadhaa ikiwemo
hatma yake kurudi CCM ambapo alisema yupo tayari kurudi iwapo Rais
Magufuli atakisafisha chama kwa kuwashughulikia wanafiki na wala rushwa Hapa chini ni maneno ya James Lembeli katika mkutano huo.
Operesheni
ya kutumbua majipu ya Rais John Magufuli nusura iwaangukie Mawaziri
wawili ambao pia walikuwa manaibu mawaziri katika Serikali ya Awamu
ya Nne.
Taarifa
kutoka katika chanzo cha kuaminiwa zimeeleza kuwa Rais Magufuli
alionesha kutoridhishwa na utendaji wa Mawaziri hao na kuwafokea mbele
ya mawaziri wenzao kwa kuwataja majina katika kikao maalum cha mawaziri
kilichofanyika hivi karibuni.
"Ni
mazingira ambayo mawaziri hawakuyazoea kwamba Rais anawaambia moja kwa
moja kwa majina, anafoka akisema anaweza kuwafukuza wakati wowote.....
"Mawaziri
wamezoea mara kwa mara wanapofanya kosa au uzembe wanaonywa kwa staili
tofauti, ni kama ya kistaarabu hivi. Sasa huyu bwana mkubwa hana mchezo,
aliwataja kabisa, tena mbele ya wenzao ambao walibaki vinywa wazi.
“Wewe (anataja jina la Waziri) na mwenzako (anamtaja jina pia) nitawatumbua,” Chanzo cha gazeti la Rais Mwema kinamkariri Rais Magufuli.
Mawaziri
hao ambao ni wabunge wa kuchaguliwa majimboni kwa upande wa Tanzania
Bara, wanaongoza wizara nyeti ambazo zinasimamia sekta mtambuka, wizara
ambazo zinagusa sehemu ya ahadi za mabadiliko alizonadi Magufuli wakati
akigombea urais katika kampeni za mwaka jana.
Chanzo
hicho kilieleza kuwa Rais Magufuli aliwaonya pia mawaziri wengine ambao
alionesha kutoridhishwa na utendaji wao kwakuwa hawaendani na kasi yake
ya kuwaletea wananchi maendeleo.
“Magufuli
alitaka atoe mfano kwa mawaziri wengine kwamba wao si watu maalum sana.
Kama wanavyotumbuliwa watu wengine na wao pia wanaweza kutumbuliwa,” kiliongeza chanzo hicho
Rais
Magufuli aliunda Baraza lake la Mawaziri mwishoni mwa mwaka jana na
kuwashauri wasifanye sherehe ya kuteuliwa kwakuwa wakifanya vibaya
hatawaonea haya atawaondoa mara moja bila kujali majina yao.
Utendaji
wa Rais Magufuli umeendelea kusifiwa kila kona hususan katika
kuwawajibisha viongozi wa ngazi zote na kuonesha nia ya dhati ya
kuwahudumia watanzania huku akipambana na uzembe na ufisad
Bado kisa na mkasa hakijabainika wazi lakini ni Shishi ndiye
aliyeanza kumtupia maneno Vee Money kwenye Instagram. Kuna uwezekano
mkubwa wawili hao walizinguana nyuma ya pazia kabla ya kuamua kuumwaga
ubuyu mtandaoni.
“Vee Jipange sana mwenzio Igunga niliaga sijaletwa kwa kubebwa kwenye
lori, nimekuja na mbio za mwenge,” aliandika Shilole kwenye post ya
Instagram ambayo imefutwa tayari. “We si wa magorofani na kiingereza
chako cha kuunga, mi ndio mtoto wa mbwa sasa maninaa,” aliongeza
Shilole.
Vanessa hakukaa kimya, alimjibu Shishi kwa post ambayo aliifuta muda
mfupi baadaye. Akipost picha ya Shishi, Vee aliandika: Nikupe Kickiii
ujulikane au sio? Kila siku twanyamaza ndio mtugaraze. Sit the f*ck
down. Mimi sio wale uliowazoea. Ps: You ain’t worth this post inashushwa
sasa hivi #MessageSent.
Haijashia hapo. Shilole amepost video akimpa ujumbe mwingine mkali zaidi muimbaji huyo wa ‘Niroge.’
“Vanessa nimepata ujumbe wako wa Kiingereza japokuwa nimeusoma kwa
tabu sana lakini nimepata baadhi baadhi,” anasikika akisema kwenye video
hiyo.
“Listen to me my sister, you see me nah, mimi mwenzio nimezaliwa
Igunga, nimezoea kula ugali, sijazoea kula chips mayai kama unavyokula
wewe. So mama ninapiga kuliko maelezo, usiombe kukutana na mimi, au
waulize wenzio waliokutana na vibao vyangu wanaweza kukuambia kwamba
kibao cha Shishi ukikutana nacho lazima uombe Panadol,” anaonya
Shishi.“Aisee bibi, bibie, bibie, I am telling you yaani usiombe
kukutana na
Bi Shishi, yaani usiombe ukakutana na mimi tit for tat, yaani mama
Kiingereza chako nimekiona, jipange, I am telling you, If I see you me
and you.”
Acha tuone movie hii itaishia wapi. Lakini kwa vitisho hivyo Vanessa hana budi kuwa na bodyguard wake sasa
ALIYEKUWA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela, (Pichani) ameibukia
kanisani na kutoa ya moyoni, ikiwa siku tano baada ya Rais Dk. John
Magufuli kutengua uteuzi wake.
Kilango, ambaye Jumatatu wiki hii
uteuzi wake ulitenguliwa baada ya Machi 20, mwaka huu, kudai kuwa mkoa
wa Shinyanga hauna mtumishi hewa wa serikali hata mmoja.
Hata
hivyo, Ikulu ilifanya uchunguzi na kubaini kuwa katika taarifa za awali
kuna watumishi hewa 45, huku kazi ya uhakiki ikiendelea katika wilaya za
Ushetu na Shinyanga.
Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa
wote, alipokuwa akiwaapisha kuwa wafanya uchunguzi kuhusu uwapo wa
watumishi hewa katika mikoa yao na kutoa taarifa.
Kutokana na
kutoa taarifa hizo zisizo za kweli, Jumatatu wiki hii, Rais Magufuli
alitangaza kutengua uteuzi wake, akiwa amekaa kwenye nafasi hiyo kwa
siku 27. Kilango amekuwa mkuu wa mkoa wa 19 tangu kuanzishwa kwa mkoa
huo.
Mbali na Kilango, Rais Magufuli pia alimsimamisha kazi
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Abdul Dachi, kutokana na taarifa
hizo za kutokuwapo watumishi hewa katika mkoa.
ALIYOSEMA KANISANI Akiwasalimia
waumini wenzake juzi, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, mjini Shinyanga,
baada ya kupewa fursa ya kusema neno, Kilango alisema anamshukuru Mungu
kwa kila jambo kwa yote yaliyomtokea.
“Ndugu waumini wenzangu,
hili ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu. Hata mtu unapojifungua mtoto
akafariki dunia, unamshukuru Mungu kwani hayo ni mapenzi ya Mungu.
"Ukiona
mzazi wako kafariki dunia pia, unamshuruku Mungu. Tunao wajibu wa
kumshukuru Mungu kwa kila jambo,” alisema kwa maneno mafupi na kisha
kuketi, huku akiacha simanzi miongoni mwa waumini wenzake, wakiwamo
viongozi wa kanisa.
ALIVYOANZA KAZI Mbele ya kikao
cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), muda mfupi baada ya kuanza kazi,
Kilango alisema Shinyanga ni mkoa wenye changamto nyingi ambazo
atazishughulikia, lakini atakuwa akilazimika kukimbia Dar es Salaam
kumwona mwenzi wake, Mzee John Malecela ambaye ni mgonjwa, na pindi hali
yake ikiimarika wataungana naye mjini Shinyanga.
Hayo aliyasema Machi 22, mbele ya wajumbe wa kikao cha kamati hiyo na Ijumaa Machi 25, alisali kanisani hapo.
Sambamba
na hayo, aliahidi kupambana na watumishi wazembe na wale wanaoendekeza
rushwa na ufisadi na kurejesha hadi ya mkoa wa Shinyanga kimaendeleo.
Kilango
ambaye yuko mjini Shinyanga, akisubiri kukabidhi ofisi kwa mrithi wake
kwa mujibu wa utaratibu, bado anaishi hotelini kwa vile aliyekuwa Mkuu
wa Mkoa huo, Ally Rufunga, hajaondoka katika nyumba ya serikali iliyoko
Ikulu ndogo, eneo la Lubaga.
ALICHOKISEMA MAGUFULI Wakati
akipokea hundi ya Sh. bilioni sita kutoa kwa Naibu Spika wa Bunge, Dk.
Tilia Ackson, Rais Magufuli alisema aliwapa wakuu wa mikoa siku 15
wakasimamie watumishi hewa, ambazo zilimalizika Machi 31, mwaka huu.
Alisema katika siku hizo 15, aliwaruhusu kufanya kazi hiyo kwa uhuru na
kuwaahidi hakutatokea kitu chochote na kwamba walifanya kazi vizuri.
Rais
Magufuli alisema watumishi hewa waliopatikana ni 5,507 ambao walikuwa
wanalipwa mishahara na miongoni mwao walikuwamo wanafunzi, waliokufa na
waliofungwa.
Alisema serikali imekuwa ikitenga Sh. bilioni 583 kulipa mishahara na kati ya fedha hizo hulipwa watumishi hewa.
“Ninaamini uchambuzi utaendelea kufanyika ili kuokoa mabilioni ya
fedha. Wizara ya Utumishi na ya Fedha muendelee kufanya kazi hiyo,”
alisema Magufuli.
Alisema zaidi ya Sh. bilioni 53 zilikuwa zinapotea kwa kuwalipa watumishi hewa 5,507.
Rais
Magufuli alisema watumishi hewa hawako katika halmashauri tu, bali wako
kila idara ya serikali, zikiwamo Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu,
vyombo vya ulinzi na usalama, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto na hata Wizara ya Fedha na Mipango.
Alisema
wakati akiwaapisha wakuu wa mikoa kwa kutambua tatizo hilo kuwa ni
kubwa, aliwapa agizo hilo na wengi waliitikia wito na kufanya kwa
ufanisi.
Rais Magufuli alisema akiwa wilayani Chato, aliona
taarifa zikitolewa na wakuu wa mikoa kuhusu watumishi hewa, lakini
alishangaa kusikia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga (Kilango), akisema katika
mkoa wake hakuna mtumishi hewa hata mmoja.
“Nilijiuliza ni
kweli? Nikatoa maagizo nikiwa Chato kuwa watu waende 'ku-verify'
(kuthibitisha) katika kila wilaya kama kweli hakuna watumishi hewa. Hadi
jana usiku (Jumapili usiku) walipatikana watumishi hewa 45 na bado
wilaya mbili zilikuwa hazijahakikiwa,” alisema.
“Niilijiuliza
sana, nikajiuliza sana na kweli nilijuliza maswali mengi kwa masikitiko
mengi kwa nini mkuu wa mkoa alizungumza vile wakati hakukuwa na adhabu
yoyote, lengo lake lilikuwa nini?
“Je, kama ni mkuu wa wilaya au
wasisidizi wake walimdanganya kwa nini na yeye alidanganya, ni shetani
gani aliyemkumba? “Nimeamua nitengue uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga
na atapangiwa kazi nyingine pamoja na katibu tawala wa mkoa,” alisema
Maguful